Mechi kati ya Coastal Union dhidi Yanga kwenye Uwanja Mkwakwani imeahirishwa.
Awali mechi hiyo ilikuwa ichezwe Jumatano, lakini sasa imeahirishwa. Hata hivyo bado haijaelezwa mechi hiyo itachezwa lini.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga amethibitisha hilo.
"Kweli nimepewa taarifa hizo baada ya timu yetu kuwa na wachezaji kwenye kikosi cha Taifa Stars Maboresho, hivyo mechi imeahirishwa," alisema Sanga.
Kutokana na hali hiyo, Yanga inaendelea na mazoezi kwa ajili ya mechi nyingi dhidi ya timu ngumu ya Polisi Moro, Jumamosi.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment