TBS YAKIPIGA ‘ STOP ’ KIWANDA CHA CHUMVI CHA SEA SALT

i wish you happy chrismass and happy new year Serikali kupitia shirika la Viwango Tanzania ( TBS ) limekifunga kwa muda kiwanda cha kuzalisha chumvi cha Sea Salt kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani kutokana na kuzalisha chumvi yenye kiwango hafifu cha madini joto. Kwa mujibu Deusdedith Paschal Ofisa Udhibiti Ubora wa TBS amesema shirika hilo limeamua kukifunga kiwanda hicho kutokana na kuzalisha chumvi kinyume na taratibu pamoja na chumvi yake kuwa na michanga, kuwa na kiasi kidogo cha madini joto ambayo huzuia ugonjwa wa goita. Akizungumzia kiasi cha madini kinachotakiwa ni miligramu 30-60 kwa kila kilogram lakini kiwanda hicho huzalisha chumvi yenye madini joto ya miligramu 14.9 katika kilo moja suala ambalo linahatarisha afya ya binadamu. Hata hivyo Deusdith amesema kuwa kiasi kikubwa kinachoonekana ni chumvi isiyoyeyuka kwenye maji hivyo kutishia usalama wa afya ya walaji. Kwa upande mwingine mkuu wa kitengo cha Mahusiano cha TBS Roida Andusamile alisema mapungufu mengine ni mmiliki wa kiwanda hicho mwenye asili ya Asia kudanganya anuani ambapo walisema kipo ubungo maziwa kumbe kipo Bagamoyo
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: