CHELSEA SAFARI WEMBLEY, YAIGONGA LIVERPOOL 1-0 NA KUTINGA FAINALI CAPITAL ONE CUP

SAFARINI kuelekea Wembley. Habari ndiyo hiyo. Bao pekee la beki Branislav Ivanovic dakika ya 94 limeipeleka Chelsea Fainali ya Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup baada ya kuilaza Liverpool 1-0 Uwanja wa Stamford Bridge, London. Chelsea inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 2-1, baada ya awali kutoa sare ya 1-1 Uwanja wa Anfield na sasa itamenyana na Sheffield United au Tottenham katika fainali Uwanja wa Wembley. Diego Costa aligombana na Martin Skrtel katika matukio tofauti wakati wa mchezo huo Stamford Bridge na mashambuliaji huyo wa Hispania alionekana mwenye bahati baada ya kugombana pia na Emre Can na Steven Gerrard, lakini hakulimwa kadi nyekundu.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: