Arsenal wamepata pigo kubwa baada ya Mastaa wao Mikel Arteta na Mathieu Debuchy kulazimika kuwa nje ya Uwanja kwa Miezi Mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji.
Kiungo Arteta, mwenye Miaka 32, aliondolewa Kimfupa kwenye Enka yake ambacho kilikuwa kikimsumbua kitambo sasa wakati Debuchy amefanyiwa upasuaji kwenye Bega aliloteguka Wikiendi iliyopita wakati Arsenal inaifunga Stoke City.
Akielezea hali hiyo, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema: “Ni bahati mbaya. Huwezi kuamini Debuchy amefanyiwa operesheni mbili katika Msimu mmoja! Ndio kwanza amerudi tu toka ya kwanza, amecheza Gemu 7 na sasa yuko nje tena!”
Mara baada ya kujiunga na Arsenal mwanzoni mwa Msimu, Debuchy aliumia na kuwa nje Miezi Mitatu na hali hiyo imemfanya aichezee Arsenal mara 14 tu tangu ajiunge toka Newcastle Mwezi Julai.
Nafasi ya Debuchy kwenye Fulbeki sasa itachukuliwa na Chipukizi Hector Bellerin au Calum Chambers.
Kuhusu Arteta, Wenger amefafanua kuwa wameamua afanyiwe operesheni wakati huu kwani maumivu ya Enka yake yalikuwa yakiathiri sehemu nyingine za Mguu wake.
Arteta, ambae mara ya mwisho kuichezea Arsenal ni Novemba 26 walipoifunga Borussia Dortmund 2-0, amefunga Bao 16 katika Mechi 136 alizoichezea Arsenal tangu ajiunge nao kutoka Everton Agosti 2011.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumamosi Januari 17
1800 Aston Villa v Liverpool
1800 Burnley v Crystal Palace
1800 Leicester v Stoke
1800 QPR v Man United
1800 Swansea v Chelsea
1800 Tottenham v Sunderland
2030 Newcastle v Southampton
Jumapili Januari 18
1630 West Ham v Hull
1900 Man City v Arsenal
Jumatatu Januari 19
2300 Everton v West Brom
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment