MBEYA CITY YAWATUMIA SALAMU ZA TAHADHARI PRISONS

Katika kuhakikisha unaivuruga Tanzania Prisons, uongozi wa Mbeya City umesema utahakikisha unacheza soka la kasi muda wote ili kuhakikisha wanapata mabao ya mapema. Timu hizo zinatarajia kukutana kesho Jumapili katika mchezo unaotajwa kuwa ni derby ya Mbeya ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya. Katibu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe, amesema sasa kikosi hicho kina morali kubwa tofauti na mwanzo ambapo walikuwa wanawachukulia poa. “Sisi tumejiandaa vizuri ili kuhakikisha tunachukua pointi zote tatu bila kujali kama timu zote ni za nyumbani au la! Awali hatukuweza kubaini matatizo ambayo yanaikumba klabu, lakini sasa kazi ya kocha imeanza kuzaa matunda hali ambayo inaleta matumaini ya kurejea kwenye chati nzuri.” Naye Kocha wa Prisons, David Mwamwaja, alisema: “Tumejindaa kuhakikisha tunashinda licha ya kuwa mvua zinanyesha sana ukanda huu.”
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: