MAPENZI:KUMBE HIZI NDIO SABABU ZA MPENZI WAKO KUTEMBEA NA RAFIKI YAKO

Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..


Ni wiki nyingine tulivu kabisa tunakutana tena kupitia safu hii nikiamini umzima bukheri wa afya na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku kama kawaida.Mimi namshukuru Muumba wa mbingu na ardhi kwa kuniwezesha kutimiza majukumu yangu ya kila siku likiwemo hili la kuelimishana na kukumbushana juu ya mambo yanayogusa maisha yetu ya kimapenzi.Mpenzi msomaji wangu, wiki iliyopitanilikuwa na kazi kubwa ya kumshaurirafiki yangu ambaye aliniletea mashitaka ya mpenzi wake kutembea na rafiki yake.Nilipata wakati mgumu sana kwani nilipoongea na msichana akaniambiawazi kwamba, amekuwa hapati penzialilotarajia kutoka kwa rafiki yangu.Msichana huyo akaenda mbele zaidi na kusema kwamba, yule shemeji yake alionesha kumjali sana kiasi kwamba siku alipomtamkia kwamba anampenda ilimuwia ngumu kukataa.Kuna kitu cha kujifunza hapa kwamba endapo utaishi na mpenzi wako bila kumdhihirishia kwamba unampenda kwa dhati, akitokea mtu wa pembeni akaonyesha kuwa kafa kaoza, tarajia kusalitiwa kama siyo kuachwa kwenye mataa.Unapokuwa umeanzisha uhusiano namtu, utambue ana watu wengi wanaomtaka lakini huenda anawakatalia kwa kuwa yuko na wewe, sasa ukionesha kutomjali, hawezi kuendelea kuwa muaminifu kwako. Atachepuka na hata kama ataendelea kuwa na wewe ni kwa kuwa labda hana ujasiri wa kukuacha.Ndiyo maana leo nikaona nikupe sababu ambazo zinaweza kumfanya mpenzi wako akatembea na rafiki yako tena wakati mwingine kwa siri bila wewe kujua. Wewe mwenyeweEndapo utakuwa umeanzisha uhusiano na mtu, wewe mwenyewe unaweza kutengeneza mazingira ya kusalitiwa. Usipoonesha kumpenda, kumjali, kuthamini penzi lake kisha rafiki yako akayaonesha hayo kwake,ni rahisi sana kukupiku.Kwa mfano, endapo umekuwa na mpenzi wako lakini hata siku moja hujawahi kumpa zawadi au kumtoa ‘out’, siku shemeji yake (rafiki yako) akiamua kufanya hivyo, mpenzi wako atahisi yeye ni mtu sahihi kwake. Kujirahisi kwakeWapo ambao wanatembea na mashemeji zao kwa sababu tu ya kujirahisi kwao. Kwa mfano unapopendelea kuzungumza mamboya chumbani na rafiki wa mpenzi wako unatarajia nini? Unapomvalia kihasara rafiki wa mpenzi wako lengo linakuwa ni lipi?Mbaya zaidi ni pale utakapokuwa na mashemeji ambao hawabipiwi. Hapanamaanisha wale ambao wakiona dalili ya kupendwa tu, wanaomba chansi

TOA MAONI YAKO HAPA

Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: