MAITI YATUPWA KITUO CHA POLISI SERENGETI MARA

Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!.. Polisi mkoani Mara imesema itawachukulia hatua askari watakaobainika kuhusu katika kifo cha Samson Nyakiha (70) baada ya uongozi wa jeshi hilo kukutana na ndugu wa marehemu waliotelekeza maiti katika Kituo cha Polisi cha Wilaya. Kamanda wa upelelezi wa makosa ya jinai wa mkoa, RCO Rogathe Mlasani alitoa ahadi hiyo katika kikao cha pamoja cha ndugu na uongozi wa polisi wa Wilaya ya Serengeti na kisha kutangaza kwa wananchi waliokuwa wamekusanyika katika kituo hicho tangu Alhamisi kusubiri hatma ya suala hilo. Katika tukio hilo, mwili wa Nyakiha aliyefia Hospitali ya Rufaa ya Bugando ulichukuliwa na ndugu ambao waliupeleka kituo hicho cha polisi na kuutekeleza, wakidai ndugu yao aliuawa kutokana na kupigwa na askari. RCO Mlasani alisema tukio hilo si la kawaida kwa kuwa limesababisha kupoteza uhai wa mtu na haliwezi kuvumiliwa kwa kuwa limekiuka misingi ya haki za binadamu. Aliwaomba wananchi wawe watulivu wakubali kuchukua mwili wa marehemu wakazike. “Naomba mliamini Jeshi la Polisi kwa kitendo kama hiki hakuna atakayelindwa, wote watachukuliwa hatua kulingana na makosa waliyoyatenda
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: