KOCHA MSAIDIZI MPYA WA SIMBA HUYU HAPA, AMEPENDEKEZWA NA KOPUNOVIC

Kocha mpya wa Simba, Goran Kuponovic amempendekeza Alphonce Gatera kuwa msaidizi wake. Kutokana na uamuzi wake huo, Gatera na Selemani Matola ndiyo watakuwa makocha wasaidizi wa Simba. "Kweli kocha amempendekeza Gatera kwa kuwa aliwahi kufanya naye kazi Polisi Rwanda. "Tulimpa nafasi ya kuteua msaidizi. Matola anendelea kubaki pia kama kocha msaidizi. Mazungumzo na Gatera yameanza na tukikubaliana, atakuja Dar es Salaam ndani ya siku chache. Gatera ni Myanrwanda aliyekulia nchini Burundi na walishirikiana vema na Kopunovic wakati akiinoa Polisi Rwanda.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: