EXCLUSIVE: YANGA YAMTEMA JUMA KASEJA KOMBE LA SHIRIKISHO

Uongozi wa klabu ya Yanga imetuma majina 23 kwa ajili ya kikosi chao kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Shirikisho lakini imemtema kipa Juma Kaseja. Katika majina majina yaliyotumwa kwenye makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf), hakuna jina la Kaseja. Caf imeipanga Yanga kuanza na BDF ya Botswana ambayo ni timu inayomilikiwa na jeshi la ulinzi la nchi hiyo. Habari za uhakika kutoka Caf zimesema, Yanga haijatuma jina la Kaseja na kusisitiza “hayumo”. “Nimeangalia, hakuna jina la Kaseja. Je, una swali jingine,” alihoji ofisa huyo wa Caf. Wakati Kaseja anasajiliwa Yanga, uongozi wa klabu hiyo ulitangaza kwamba zaidi umemsajili kwa ajili ya michuano ya kimataifa. Lakini hivi karibuni aliingia kwenye mgogoro na uongozi wa Yanga baada ya kudai amecheleweshewa malipo yake na Yanga ilikuwa imevunja mkataba. Kaseja aliipelekea Yanga barua akitishia kufungua kesi mahakamani, halafu malipo yake yakafanyika. Baada ya kulipwa, aliiandikia Yanga barua nyingine akiiambia kwamba amepokea fedha zake na yuko tayari kuendelea kuitumikia. Hata hivyo Yanga haikuwahi kumjibu lolote, zaidi ya kukaa kimya na Kaseja amekuwa kimya pia.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: