Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
Zitto Kabwe ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, mwanzoni mwa 2014 kulikuwa na mgogoro kati yake na Chama cha CHADEMA.
Magazeti mengi yaliyotoka siku chache zilizopita yaliripoti taarifa ya Mbunge Zitto Kabwe kurudi tena CHADEMA, hali iliyomfanya Zitto afunguke kuhusiana na ishu hiyo.
“Hapana nadhani hizo ni tetesi kwa sababu sijatoa kauli yoyote kuhusiana na hilo na moja mimi bado mwanachama wa Chadema kwa sababu nina kesi mahakamani na kesi hiyo haijaamuliwa,bado inaendelea.
“Sijawahi kutoka kwenye uanachama wa CHADEMA, mtu anaposema nataka kurudi Chadema hayuko sahihi, inafahamika nilikuwa na matatizo na chama hatujaweza kuyatatua, hakuna mazungumzo yoyote ambayo yamefanyika lakini kuna baadhi ya watu wameanza kuleta hayo mazungumzo“– Zitto Kabwe.
0 comments:
Post a Comment