Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!.. Balozi wa Marekani Mark Childress na Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, Lazaro Nyalandu wakitiliana saini mkataba wa Marekani kuipa Tanzania msaada wa vifaa pamoja na mafunzo kukabiliana na ujangili nchini Tanzania. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia wizara ya Mali Asili na Utalii leo imepata msaada wa vifaa vya kukabiliana na ujandili kutoka serikali za Marekani na Ujerumani katika hafla iliyofanyika leo katika Mbuga ya wanyamapori ya Selous. Walio kabidhi vifaa hivyo ni Balozi wa Marekani Tanzania Mark Childress pamoja na Balozi wa Ujerumani Tanzania Egon Kochanke. Wote kwa pamoja na wametiliana saini mkataba na Waziri wa Mali Asili na Utalii Lazaro Nyalandu ambapo nchi hizo zimekubaliana kuipa Tanzania msaada wa vifaa vya kisasa vya kukabiliana na majangili katika mbuga ya wanyama ya Selous. Katika hatua nyingine serikali hizo zitatoa pia msaada wa mafunzo yakiwemo ya kikomandoo kwa askari wa wanyamapori ili kukababiliana na wimbi la ujangili nchini Tanzania.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: