i wish you happy chrismass and happy new year Mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara kati ya Mbeya City Fc na Yanga uliokuwa umepangwa kuchezwa jumamosi hii kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya umeahirishwa kupisha mashindano ya Kombe la mapinduzi. Kwa mujibu wa taarifa kutoka shirikisho la soka nchini TFF, michezo mingine yote iliyokuwa inazihusisha timu za Simba, Azam na Mtibwa ambazo nazo zitashiriki michuano hiyo pia imesogezwa mbele. Hii ndiyo taarifa ya TFF Kwa vile klabu nne za Azam, Mtibwa Sugar, Simba naYanga, timu zao zitashiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoanza Januari 1mwakani kisiwaniZanzibar; mechi zifuatazo za LigiKuu ya Vodacom (VPL)zitapangiwa tarehe nyinginekatikati ya wiki. Mechi husika ni namba 59 (Azam vs Mtibwa Sugar-03.01.2015), namba 61 (Mbeya City vs Yanga- 03.01.2015), namba 62 (MgamboShooting vs Simba-04.01.2015). Mechi nyingine ni namba 66 (Coastal Union vsYanga- 10.01.2015), namba 67 (Kagera Sugar vs Azam- 10.01.2015), namba 68(Simba vs Mbeya City- 11.01.2015) na namba 69 (Mtibwa Sugar vs TanzaniaPrisons- 11.01.15). Boniface Wambura Mkurugenzi Idara ya Mashindano Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: