Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Yanga, Said Bahanuzi, amewatahadharisha Yanga kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya timu yake ya sasa Polisi Morogoro mchezo unaosubiriwa kwa hamu kubwa kunako Uwanja wa Jamhuri.
Bahanuzi ambaye ameenda Polisi Moro kwa mkopo katika dirisha dogo la Usajili, amesema kuwa kwa sasa anamapenzi na timu yake hiyo anayoitumikia kwa sasa hivyo amewataka mashabiki wajitokeze kwa wingi kuangalia Yanga wakifia Jamhuri.
“Wasitegemee kupata matokeo kirahisi, Tumejipanga kupata pointi tatu, Mashabiki wajekuona vijana nini tunacho” Amesema Bahanuzi.
Yanga inayonolewa na kocha Hans Van Der Pluijm waliondoka jana Jijini Dar es salaam na kutua Morogoro tayari kwa mchezo huo hapo jioni ya leo ikiwa ni mchezo wa raundi ya 12 ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara (VPL).
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment