ALIYETANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS KUPITIA CCM ARUKWA AKILI ,APELEKWA KWA WAGANGA WA KIENYEJI
katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Bariadi, kwa sasa amepata matatizo ya akiri na kualazimika kupelekwa kwa wataalamu wa kienyeji ili kuweza kupata matibabu yapata miezi 3 sasa hajapona.
Taarifa zilizopatika ndani ya Chama cha Mapinduzi Wilayani hapa, zinabainisha kuwa kiongozi huyo Masunga Lyabuyenze ambaye pia alikuwa katibu wa Mbunge Andrew Chenge alipelekwa kwa wataalamu hao baada ya kuonekana hali yake siyo swari.
Hata hivyo vyanzo hivyo vya habari ambavyo havikutaka kutajwa majina yao katika mtandao huu, vilibainisha kuwa, hatua ya kumpeleka kiongozi huyo, ilichukuliwa na Mbunge huyo ambaye alitajwa katika kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya Bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow.
Hata hivyo kabla ya kupelekwa kwa wataalamu hao, kigogo huyo baada ya kutangaza kuwania nafasi ya urais, hali yake ilianza kuonekana kwa kunywa pombe mara kwa mara, kutembea huku akiwa anAongea peke yake, kukaa ameshikiria vitabu na magazeti, pamoja na kuvaa kaptula kila mara wakati ni kiongozi mkubwa ndani ya chama tawala.
Baadhi ya wananchi wanaofuatilia siasa ndani ya wilaya hiyo walimweleza mwandishi wa mtandao huu, kuwa chanzo cha kigogo huyo kupata matatizo ya akiri ni kutangaza nia ya kugombea uraisi, wakati uwezo wake ni mdogo.
"...ndani ya CCM wanaotangaza nia ni watu wakubwa kama mnaona hata nyie waandishi wa habari..sasa huyu bwana kila siku tunaishi naye hapa kwenye kahawa, mitaani, alafu anaamka asubui anatangaza nia ya kugombea wewe unafikiri hao wakubwa watamuacha" Alisema mmoja wa wanaharakati.
Mpaka sasa yapata muda wa miezi 3 kiongozi huyo amepelekwa kwa wataalamu hao wa kienyeji kwa ajili ya kupata matibabu na kurejea katika hali yake ya awali.
0 comments:
Post a Comment