ZITTO KUIBUA KASHFA KUBWA ZAIDI YA ESCROW 2015

Sakata lingine litakalohusu kashfa nne kubwa zaidi ya ESCROW kuibuka mwakani kufuatia kamati ya Bunge ya Hesabu za serikali (PAC) kukamilisha ufisadi uliofanyika katika akaunti ya Escrow. Katika sakata hilo Bunge limetaka serikali kuwawajibisha Mawaziri pamoja na watendaji wa serikali na kuendeleza uchunguzi kwa waliopata mgao wa fedha ambazo ni zaidi ya bilioni 306. Kwa mujibu wa Mwenyikiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Zitto Kabwe amesema kwamba kamati yake itatumia mwezi desemba na januari mwakani kupitia ripoti nne ambazo zina maslahi kwa Taifa. Akinzungumzia kashfa hizo, Zitto amesema kuwa kashifa hizo ni za utoaji vibali vya kuagiza sukari na kuingiza sukari nchini, ripoti nyingine ni uchunguzi wa ubinafsishaji wa Benki ya NBC, ripoti maalumu ya Bandari pamoja na mikataba ya gesi. Sakata la utoaji wa Vibali vya sukari, imebainika kuwa ufisadi wake ni mkubwa kuliko hata sakata la ESCROW lilionekana kuteka hisia za watanzania kwa takribani wiki moja. Hatua hiyo inatokana na baadhi ya wamiliki wa viwanda vya sukari nchini Tanzania kutangaza kuwa wana mpango wa kuvifunga viwanda vya sukari kutokana na kuviendesha kwa hasara kwa kuwa kuna ushindani mkubwa wa soko la sukari kutokana na kuruhusu wafanyabiashara kuingiza kutoka nje ya nchi
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: