YANGA SC YALETA BONGE LA STRAIKA LA LIBERIA LINALOCHEZA CYPRUS

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Liberia, Kpah Sherman anatarajiwa kutua usiku wa kuamkia kesho kwa ajili ya kufanya mpango wa kujiunga na klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam. BIN ZUBEIRY inafahamu Kpah anatarajiwa kufikia vipimo vya afya ambavyo akifuzu atapewa Mkataba wa mwaka mmoja, baada ya mazungumzo ya awali na uongozi wa klabu hiyo. Kpah Sherman mwenye umri wa miaka 22 anakuja Yanga SC akitokea klabu ya Cetinkaya ya Ligi Kuu ya Cyprus Kaskazini, ambako analazimika kuvunja Mkataba wake uliobakiza miezi minne. Kpah Sherman anakuja leo Dar es Salaam kwa mipango ya kujiunga na Yanga SC Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali kwenye mitandao, Sherman anaonekana ni mshambuliaji hatari na kijana mdogo, ambaye kama Yanga SC wakifanikiwa kumpata na akabahatika kung’ara katika soka ya Tanzania, watakuwa wamelamba ‘dume’. Alianza kuichezea Cetinkaya mwaka 2012, akitokea Duzkaya SK aliyoanza kuichezea mwaka 2010, akitokea Barrack YC ya nyumbani kwao, Liberia ambayo alianza kuichezea mwaka 2009. Sherman akifanikiwa kusaini Yanga SC, atakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa dirisha la dogo baada ya kiungo mkabaji Mbrazil, Emerson de Oliviera Roque na mshambuliaji mzalendo, Danny Mrwanda aliyekuwa anacheza Vietnam. Kaph Sherman akiichezea timu ya taifa ya Liberia Hata hivyo, kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu Yanga SC kama itamsajili Sherman mkali wa mabao katika Ligi ya Cyprus Kaskazini, italazimika kukata mchezaji mmoja wa kigeni ili ikidhi kanuni ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inayotaka wageni watano tu. Bila ya Sherman, tayari Yanga SC inao Wabrazil Emerson, Andrey Coutinho, Wanyarwanda Haruna Niyonzima na Mbuyu Twite na Mganda Hamisi Kiiza. Na kama Sherman atafanikiwa kusajiliwa Yanga SC atakuwa Mliberia wa pili kucheza Tanzania, baada ya William Fahnbullar aliyewika Simba SC kuanzia 1997 hadi 1999 alipohamia Kajumulo WS kabla ya kutimkia Ulaya @bin zubery
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: