WAUMINI WAMKATAA MCHUNGAJI WAO HUKO BUKOBA, WALETA FUJO KANISANI, IBAADA YAAHIRISHWA
Kama hukusikiliza Hekaheka ya Jumanne ya Desemba 9 kupitia Clouds FM kwenye Leo Tena, inahusu Waumini wa Kanisa laTAGBukoba kumkataa Mchungaji mpya aliyeletwa Kanisani hapo kwa madai ya kumtaka Mchungaji aliyehamishwa na kupekwa sehemu nyingine arejeshwe.
Baada ya Waumini kumaliza Kuabudu kwa Nyimbo Mchungaji huyoPius Alphoncealiinuka na kuanza Kuhubiri ndipo baadhi ya Waumini walipoamka na kusema kuwa hawawezi kuendelea na Mahubiri kutokana na watu wachache wanaotaka kulivunja Kanisa hilo kwa maslahi yao binafsi, hivyo kutaka Mchungaji wa zamaniErius Manotialiyehamishiwa Karagwe arejeshwe.
Hali hiyo ilipelekea mahubiri hayo kusimama na kuzuka fujo na kusababisha ibada hiyo kuahirishwa.
0 comments:
Post a Comment