WATUHUMIWA FEDHA ZA ESCROW WANG’ANG’ANIWA KILA KONA

Watuhumiwa waliohusika katika upotevu wa zaidi ya bilioni 306 wanazidi kuandamwa na wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wa kisiasa. Wananchi hao wameitaka serikali kuhakikisha kwamba wanavuliwa nyadhifa na kurejesha fedha zote walizogawana. Watuhumiwa katika sakata hilo ni Waziri wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo na naibu waziri wake Stephen Masele, Eliakim Maswi, Mwanasheria mkuu wa serikali Jaji Fredrick Werema pamoja Waziri wa Nyumba Ardhi na maendeleo ya makazi Prof. Anna Tibaijuka. Akizungumza na wananchi mjini Musoma, Naibu Waziri wa Fedha Ndugu Mwigulu Nchemba amesisitiza kuwa ni lazima hatua kali za kinidhamu zichuliwe kwa wahusika wote waliohusika na sakata la Escrow kama ambavyo Bunge limependekeza. Kwa upande wa Wananchi katika mahojiano na Mwandishi wetu wa Habari wamelipongeza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweka tofauti zao kando na kuungana katika kuhakikisha kwamba wale waliosika katika sakata hilo wanachuliwa hatua ili iwe fundisho kwa watendaji wengine wa serikalini. Kwa upande mwingine ufisadi uliofanywa na vigogo serikalini ni kushirikiana baina ya Harbinder Singh Sethi ambaye ni mfanyabiashara mwenye asili ya bara la Asia aliyekuwa anamiliki mtambo wa wa kampuni ya kufua umeme wa IPTL.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: