WABAKAJI WAKAMATWA NA POLISI WAKIWA ENEO LA TUKIO
Polisi wa kituo cha Kiamumbi Kenya wamewakamata washukiwa watano katika maeneo ya Githurai baada ya binti mmoja kubakwa akiwa anaelekea nyumbani akiwa ameongozana na rafiki yake wa kiume ambapo walipofika karibu na msitu huo walivamiwa na msichana huyo kubakwa na wanaume watano.
Msichana huyo ambaye amefanyiwa kitendo hicho amesema; “…wakatuuliza umeona ng’ombe hapo huyo boy akasema hapana hatujaona ng’ombe, kisha wakatuambia ooh… wakatokea side hii na mwingine side hii… wakasema laleni chini , niliacha yule boy amevuliwa nguo amefungwa mikono mie wakanipeleka place nyingine pamoja naye ila hatukuwa pamoja vile tumeenda ndio akaniwekea ile nguo kwa macho nisiwaangalie ndio wakaaanza mambo yao kila mtu walikuwa watano wananifunga mikono nyuma na miguu…”
Baadaye majambazi hao walimuacha msichana huyo na kumleta mvulana aliyekuwa naye ambapo binti alipata nafasi ya kuwakimbia kwenda kutoa taarifa.
Msako iliofanywa ulifanikiwa kufika kwenye pango la wezi hao na kufanikiwa kuwakamata wote watano wakiwa na vitu nguo za wanawake , kadi za ATM, vitambulisho vya wanawake ambao wamewahi kuwafanyia kitendo hicho.
Moja ya watuhumiwa waliokamatwa eneo hilo amesema; “mimi naitwa Peter Kong’o nimeokoka… Kristo ni Bwana na Mwokozi wangu .. nakujaga kusali pale Wichu karibu na njia manake mimi nimeokoka na nikisali napataga ushindi na ufufuo”
Polisi walichoma vitu walivyovipata na washukiwa wote watano wamepelekwa kituoni ili kufanya uchunguzi zaidi.
0 comments:
Post a Comment