UMEONA MAANDAMANO HAYA YA KUPINGA UKEKETAJI? HEBU ANGALIA

Jivunie kuwa mwana ludewa


Ukifika nje ya geti la Kituo cha Masanga tangu mwezi huu wa 12 ulipoanza utakutana na huu ujumbe ''HAKATWI MTU HAPA'' hiki ni kituo cha kuzuia ukeketaji (TFGM) ambacho kinatoa mafunzo ya ukeketaji mbadala na tohara salama... kwa sasa kuna watoto zaidi ya 600 ambao wamekimbilia hapa ili wasikeketwe tangu msimu huu ulipoanza mwezi wa 12/2014...

Mwezi wa 12 ni mwezi wa kufanya tohara mkoani Mara ambapo watoto wengi huwa wamefunga shule na hivyo kupelekea watoto wa kike hukeketwa...
Pata mwonekano wa Kituo cha Masanga, ambacho kipo katika kijiji cha Masanga Wilaya ya Tarime Mkoa wa Mara...
Kituo hiki cha Masanga kinategemea sana maji ya mvua, na mvua hazijanyesha siku za karubuni, jmosi iliyopita waliletewa maji na Mkuu wa Wilaya ya Tarime.... kwa hiyo wanahitaji msaada wa haraka sana sana...
Mabango haya yamebeba ujumbe tofautitofauti kwa lengo la kuifikishia jamii kilio chao kutokana na hii mila yao ya Ukeketaji...
Niliwatia moyo kwamba wakati mwingine inabidi wasisubiri kufanyiwa MAAMUZI hasa yale maamuzi yenye madhara kama hii mila ya Ukeketaji...
Watoto waliokimbilia kituo cha Masanga kujiokoa na kisu cha msumu huu wa Ukeketaji mkoani Mara...
Watoto zaidi ya 600 wakitoa sauti zao kupinga kukeketwa mwezi huu wa 12/2014.. wanahitaji msaada wa dharura kama Maji, chakula, pedi, n.k
Watoto wakitoa sauti zao nje ya kituo cha Masanga kuieleza jamii ya Tanzania na Dunia nzima juu ya Mila yao ya Ukeketaji ambayo inawakandamiza wasichana kwa kiasi kikubwa...
Nimeona ni busara kuwaomba Umma tushirikiane kuwasaidia watoto hawa hasa kipindi hiki kigumu ambacho wamekimbia kukeketwa wakingojea msimu uishe mwezi huu wa 12 warudi makwao wakaendelee na shule... yaani hawana hata maji! kama ujuavyo maji ni muhimu sana kwa binadamu, na huwa wanategemea maji ya mvua!!! sasa mvua hazijanyesha hivi karibuni... pia hawana chakula, pedi, nguo, viatu, kama una maswali zaidi unaweza kumuuliza mkuu wa kituo hicho Sister Germana... Lakini chondechonde nakuomba tuwasaidie wako kwenye hali mbaya...
Msimu wa Ukeketaji ukiendelea, Watoto hawa wametoka kukeketwa.... baadhi ya watoto wamekimbilia kituo cha Masanga...
Msimu wa ukeketaji ndo umepamba moto Trime...wakati watoto zaidi ya 600 wakitorokea Masanga, huku wengine wanaendelea na Tamasha la Ukeketaji kama kawaida.... Kikubwa ni kutoa elimu kwa jamii juu ya mila hii inayomkandamiza mtoto wa kike... Lakini kwa sasa tuwaokoe watoto wetu na hali iliyopo hivi sasa....
Nilipata wasaa wakuongea na Wazee wa Koo 13 Tarime juu ya hii mila ya Ukeketaji na jinsi hali halisi ilivyo...
Wawakilishi wa Wazee wa Mila Koo 13 Tarime.... mengi utayasikia kwenye kipindi cha @wanawakelive ila kwa sasa MSAADA WA HARAKA UNAHITAJIKA....
Huyu ndo Mkuu wa kituo kile cha Masanga chenye wasichana zaidi ya 600 waliokimbia kukeketwa, anaitwa Sister Germana.... Namba zake zipo kwenye bana lenye maandishi ya kuomba msaada wa dharura....
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: