TACAIDS:‘ NJOMBE KINARA KWA MAAMBUKIZI YA UKIMWI TANZANIA

Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani kitaifa yanafanyika leo mkoani Njombe. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids) 2011/12, Mkoa wa Njombe, Mbeya na Iringa ni vinara wanaoongoza kwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini huku Pemba na Unguja zikiwa chini kwa maambukizi hayo. Aidha, mkoa wa Njombe unaongoza kwa maambukizi ukiwa na asilimia 14.8, ukifuatiwa na Iringa wenye maambukizi asilimia 9.1 na Mkoa wa Mbeya unashika nafasi ya tatu kwa asilimia 9. Mikoa mingine na asilimia za maambukizi katika mabano ni Shinyanga (7.4), Ruvuma (7.0), Dar es Salaam (6.9) Rukwa (6.2), Katavi (5.9), Pwani (5.9),Tabora (5.1), Kagera (4.8) na Geita (4.7). Mikoa mingine aliyoitaja ni Mara (4.5), Mwanza (4.2), Mtwara (4.1), Kilimanjaro (3.8), Morogoro (3.8), Simiyu (3.6), Kigoma (3.4), Singida (3.3), Arusha (3.2), Dodoma (2.9), Lindi (2.9), Tanga (2.4), Manyara (1.5), Unguja (1.2) na Pemba (0.3). Wanawake wana kiwango kikubwa cha maambukizi kuliko wanaume mijini na vijijini. Asilimia 7.2 ya wakazi wa mijini wana maambukizi ya VVU ukilinganisha na asilimia 4.3 ya wakazi wa vijijini. Kwa upande wa Tohara kwa wanaume, Tume ya ukimwi imebainisha kuwa takwimu zimeonyesha inapunguza maambukizi ya Ukimwi kwa asilimia 60 na kusisitiza kuwa ipo haja ya kutoa elimu zaidi juu ya uelewa wa ugonjwa huo. Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani isemayo, Tanzania Bila Maambukizi Mapya ya VVU, Vifo Vitokanavyo na Ukimwi na Ubaguzi na Unyanyapaa inawezekana inayolenga kupunguza maambukizi Mapya ya Ukimwi, kupunguza vifo vitokanavyo na Ukimwi na kukomesha vitendo vya unyanyapaa kwa asilimia Sifuri.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: