PROMOTA WA NGUMI TANZANIA AFUNGIWA
Promota wa Mpambano wa Ubingwa wa UBO Kaike Siraju katikati akiwanyoosha mikono juu mabondia Ramadhani Shauri kushoto na Cosmas Cheka.
Kamati ya muda ya Shirikisho la ngumi za kulipwa Tanzania TPBC imeamua kumfungia kwa muda promota wa mchezo huo Kaike Silaju kufatia dhuruma aliyoifanya dhidi ya Mabondia na maafisa wa mchezo wa ngumi.
Akizungumza na mwandishi wetu mwenyekiti wa kamati hiyo Chausiku Palasa ameema kuwa promota huyo amefungiwa kwa miezi mitatu asijihusishwe na maswala ya ngumi hadi atakapolipa madeni hayo.
Ameongeza kuwa makosa aliyofanya promota huyo ni pamoja na kutowalipa mabondia waliopigana katika mpambano wa 21 Agosti mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri Morogoro, Pili alishindwa kuwalipa fedha maafisa wa mchezo huo ikiwa ni pamoja na kuutelekeza ukumbi huo.
“Tumekuwa tukimwambia alipe fedha hizo lakini anatuambia atalipa hivyo kupitia mkutano wa kamati tuliokaa jana Septemba 31 tuliamua kumfungia hadi atakapolipa madeni hayo” Amesema Palasa
0 comments:
Post a Comment