NJOMBE KINARA WA MAAMBUKIZI YA UKIMWI KITAIFA
Ikiwajanani siku ya UKIMWI, Duniani ambapo Tanzania Kitaifa siku hiyo inafanyika Mkoani Njombe Juhudi za kupambana na maambukizi ya ukimwi mkoani humo zimezidi kushika kasi kutoka katika mashirika mbalimbali na kuanza kuungana na viongozi wa mila
Akizungumza na mwandishi wetu katika viwanja vya Sabasaba mkoani njombe, afisa uhusiano wa PSI kanda ya njanda za juu kusini, Sanday Beebwa amesema kuwa katika vitu vinavyo ongeza kasi ya maambukizi mkoani humo na Tanzania kwa ujumla ni pamoja na tamaduni na mila.
Beebwa amesema sasa wameanza kushirikiana na viongozi mbalimbali wa dini na viongozi wa kisiasa ambao wanawasihi kutoa elimu kwa wanachi wanapo kutana nao popote pale katika mikutani yao.
Aidha Beebwa ameongeza kuwa katika mikoa mitano ya juu Mikoa ya Nyanda ndio inaongoza huku mkoa wa njombe ukiwa ndio mkoa pekee Tanzania wenye tarakimu mbili za Kitakwimu katika Maambukizi
Maadhimisho haya kilele chake nijanaambapo mgeni rasmi alikuwa makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
0 comments:
Post a Comment