Njenje News blog: ONE DAY YES sehemu ya 1 b
karibu na mke wangu kwa kumtunza uzazi nini na nini... daah nazani mnajua hivyo tusiliongelee sana....
Mke wangu nampenda sana tena toka alivyonizalia mtoto ndio nilizidi kumpenda zaidi pamoja na saidi wangu
Sasa wakiwa wake zetu wapo mbele na sisi tulikua nyuma.. hio ni baada ya kuvuka korongo moja hivi lenye kupitisha maji machache sana...
Nilichomwa na mwiba mkubwa tu mguuni... maana vijijini kutembea peku sio jambo la kushangaaa
Sasa ikabidi nichuchumae ili niutoe ule mwiba maana damu nyingi zilikua zikitoka,
"nini rashidi? umefanya nini tena?"
Ni broo wangu aliniuliza kihivyo
"ni mwiba tu usjali kaka"
Basi tuliseidiana kutoana na wakati ho nae mke wangu kaja mbio huku akiuliza kuna nini. Alipoona damu zinatoka kwangu ilibaki tu kidogo azimie afu na vile alikua ana mtoto mgogoni sijui ingelikuaje kwakweli....
sasa baada broo wangu kumzuia na kumueka chini... nilimuelezea kilichotokea huku nikijitahidi kusimama... basi niliutoa mwiba ule kisha nikawa najitahidi kusimama... basi tukaanza kupiga hatu za kuelekea nyumbani, Sasa kabla sijamalizia hatu kadhaa niliskia
"vuuuuuuu"
Kwa nyuma yangu, lakini sikuona mtu kabisa
"broo we ndio merusha jiwe huku nyuma?"
"jiwe? saa ngapi nilishika jiwe?"
"au ni wewe shemu nini?"
Nilimuuliza mke wa broo kiutani tu. sasa kabla sijapiga tena hatua niliskia tena ile sauti.. ya mtu kupita kwa spidi nyuma ya mgongo wangu
"Broo tuache masihara bwana mbna mnarusha mawe?"
"nani karusha mawe wewe?"
"ok poa twendeni"
Tulianza safari huku tukipiga stori za hapa na pale
Lakini ghafla niliguswa usogoni mithili ya mtu alienisodoa...
"aiseee broo mbona mi sielewi?"
"nini wewe?"
"nani kanigusa kwa nyuma?"
"sasa mimi nipo mbele nitakugusaje kwa nyuma?"
"eeeehh??"
"Eeenhh eee eee Eeee nini sasa?"
"eeee?"
"nitakutia makonzi rashidi sitaki mchezo"
"eeeee?"
Sasa ilikua naitikia tu eeee bila kujielewa kua ninachokifanya sicho
Ilifikia mahari nimelitupa jembe kisha nikaanza kurudi nyuma tena nikielekea kle korongoni tulipo papita mwanzo
"we chidi unaenda wapi uko?"
Nilikua simsikilizi mtu huku bado nikiwa naitikia eeee kama vile kuna mtu alikua ananiita hivi...
"we chidi twende bhana unaenda wapi huko?"
Mara mke wangu akamuuliza broo
"ana nini yule?"
"mi sijui ndio namuoa sasa hivi"
"sasa si umfatilie jamani shemeji"
"aaaa huyu ana utani sana uyu usikute anatuchezea tu"
"jamani shemeji nenda kamuangalie"
"au anaenda kunywa maji nini?"
"mmhh toka lini akanywa maji ya korongoni?"
"mi sijui kwani si mumeo"
Sasa nilipokua naeda kulikua na korongo kubwa tu...ambalo nikidondokea huko basi na kifo ni huko huko...
Nilifika hadi mwisho wa lile korongo... yaani nikipiga hatua tu basi tena na sitokua mimi tena...
Sasa nilipofika hapo nilishindwa kujua pa kuelekea hivyo.. nilibaki tu nikiwa nimesimama pale
ghafla Kulidondoka jani la mti lakini sio jani kama jani... bali lilikua na ujumbe fulani..
Nililiokota na kulifungua kwa haraka
Heeeeeee nilishangaa kilichoandikwa humo kwenye hicho kijani
Eti kimeandikwa hivi
"usi.................
Gonga like iendeleeeee
0 comments:
Post a Comment