HALMASHAURI YA LUDEWA YAVUNJA MKATABA NA WANANCHI UJENZI WA MADUKA YANAYOZUNGUKA UWANJA WA MPIRA

Na barnabas njenjema ludewa
Baadhi ya  maduka  yaliyokuwa  yakijengwa  eneo la  uwanja  wa  mpira na mikutano wa mjini Ludewa ambayo kwa  sasa yamesitishwa  kujengwa  na halmashauri  kuanza  kurudisha  fidia kwa  kila mwenye jengo eneo hilo ambalo  awali  mkakaba  ulikuwa ni  wananchi kujenga na  kwa  kipindi  cha miaka mitano ya kuendesha  hao  wananchi hao  wangekuwa  wakilipa  nusu kodi na baada ya   kurudisha  gharama  zao  za  ujenzi  basi wangekuwa  ni  wapangaji kwa Halmashauri  hiyo

 Sehemu ya maduka  ambayo yalianzwa  kujengwa  hapo 

 Kutokana na  kuvunjwa kwa mkataba  huo  hivi  sasa  Halmashauri  itajengwa maduka  hayo kwa gharama  zake na  kukodisha kwa  bei  kulingana na  wakati  husika   ili  kukuza mapato ya  Halmashauri  hiyo ambayo kipato chake ni  chini  zaidi


 

 Baadhi ya maduka yaliyokuwa yakijengwa eneo la uwanja wa mpira na mikutano wa mjini Ludewa ambayo kwa sasa yamesitishwa kujengwa na halmashauri kuanza kurudisha fidia kwa kila mwenye jengo eneo hilo ambalo awali mkakaba ulikuwa ni wananchi kujenga na kwa kipindi cha miaka mitano ya kuendesha wao wananchi hao wangekuwa wakilipa nusu kodi na baada ya kurudisha gharama zao za ujenzi basi wangekuwa ni wapangaji kwa Halmashauri hiyo. Hata hivyo HALMASHAURI ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe yaanzakurejesha fedha zaidi ya Tsh mlioni 68 kwa wananchi wake baada ya kuvunja mkakaba kandamizi kwa uchumi wa Halmashauri huo kati yake na wananachi hao baada ya kubaini kupata hasara kubwa zaidi . Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Bw Wiliam Waziri ameueleza mtandao huu wa njenje news blog leo kuwa hatua ya kurejesha fedha hizo ambazo ni kiasi cha Tsh milioni 3 kwa kila mmiliki wa jengo ene hilo la uwanja wa mpira na ule wa mikutano mjini Ludewa baada ya wananchi waliokuwa wakijenga hapo kuonyesha kugeuka makubaliano ya mkataba . Alisema kuwa kwa mujibu wa mkataba wananchi hao walipaswa kujenga kwa gharama zao na kwa kipindi cha miaka mitano wangeweza kurehjesha gharama zao kwa kulipa kodi ya nusu kodi na nusu ya kodi hiyo kuweza kuingia katika mapato ya Halmashauri na baada ya miaka mitano ya kurudisha gharama zao basi wangeingia mkataba upya kama wapangaji ambao wangeanza kulipa kodi kulingana na viwango pendekezi vya kodi ya Halmashauri. "Tumelazimika kuvunja mkabata huo baada ya kuona wananchi wameanza kukiuka makubaliano mapema na iwapo tutaacha hivyo yawezekana Halmashauri kukosa mapato yake kama ilivyo katika maduka ya sokoni ambayo pia mkataba ulikuwa kama huu ila baadae waligeuka na kulipa kodi ya Tsh 15000 kwa mwaka " Hivyo alisema katika kuepusha mapato kuendelea kukosekana katika Halmashauri hiyo ambayo hadi sasa haina chanzo cha uhakika cha mapato wamelazimika kuvunja mkakaba huo na kurejesha gharama walizotumia kwa kila mmoja na kuzirejesha ili zoezi la kujenga maduka hayo lifanywe na Halmashauri. Vibanda hivyo ambavyo baada ya kusimamishwa na halmashauli kuelea kujengwa kwa sasa ni magofu kwan vimejengwa nusu na kuleta hali mbali ya mzingira mjini hapa. Baadhi ya wafanyabiashara wakiongea na njenje news blog wameiomba halmashauli hiyo ya wilaya kufanya haraka kukarabati vibanda hivyo kwani kutachochea maendelea ya wilaya ya ludewa pamoja na mkoa wa njombe kwa ujumla, miaka hamsini na tatu ya uhuru ludewa bado hatuna huduma bora ambayo mwana ludewa atajivunia kwa upande wa biashara,..
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: