MWANAMKE AIFICHA NDANI MAITI YA MUMEWE KWA MUDA WA MIEZI 6

Huwa inakuwa ngumu kuamini kinachoendelea pale ambapo mtu ambaye unampenda sana inapotokea anafariki. Tumeshuhudia matukio ya ndugu zetu wengi kufariki na kutuacha kwenye wakati mgumu, labda ndiyo sababu ambayo hata huyu mwanamke Kaling Wald wa Canada kuuhifadhi mwili wa maiti ya mume wake chumbani cha kulalia kwa muda wa miezi sita akiamini kuwa Mungu atamfufua. Mwanaume huyo Peter aliugua ugonjwa wa Kisukari lakini hakutumia tiiba yoyote kutokana na kutotumia dawa yoyote akiamini atapona kwa njia ya maombi aliyokuwa akiyafanya ambapo muda mfupi baadaye hali yake ilibadilika ambapo alipoteza fahamu na kufariki. Mke wa marehemu na Watoto wake watano waliamini kwamba Peter angefufuka, wakaamua kufunga mlango na kufanya maombi ili afufuke. Serikali iligundua tukio la kuwepo mwili huo ambao ulikuwa tayari umeoza ndani ya nyumba hiyo mwezi Septemba walipofika nyumbani kwa Wald kuwafukuza kutokana na mikopo waliyokuwa wanadaiwa. Wald alikiri kushindwa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika juu ya kifo hicho na kwa mujibu wa sheria alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela na miezi 18 ya kupatiwa ushauri nasaha.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: