MWANAFUNZI AJIFUNGUA MTOTO KWENYE CHOO CHA HOSPITALI YA KCMC NA KUMTUPA KWENYE NDOO YA TAKATAKA
Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Utabibu Moshi amejifungua mtoto katika choo cha Hospitali ya rufaa KCMC na kisha kumtupa mtoto wake kwenye kasha la takataka.
Tukio hilo ambalo limezua gumzo kubwa mjini Moshi lilitokea juzi asubuhi katika choo kilichopo mapokezi ya wagonjwa waliozidiwa.
Habari kutoka katika hospitali hiyo zinasema mwanafunzi huyo ambaye kwa sasa jina lake limehifadhiwa ambaye anasoma mwaka wa kwanza anasomea masomo ya matibabu yamazoezi ya viungo.
Mwanafunzi huyo alifika eneo la mapokezi akiwa na mwanafunzi mwenzake na akaingia chooni kwa lengo la kujisaidia na baada ya muda muhudumu wa usafi aliingia na kukuta choo kimetapakaa damu na baadaye kusikia sauti ya mtoto akilia kutoka kwenye pipa la taka lililopo ndani ya choo hicho.
Alipochungulia alikutana na mtoto mchanga ambaye alikua hata hajakatwa kitovu na inasemekana mwanafunzi huyo alikwenda pale baada ya kusikia ana maumivu ya tumbo na kwa sasa wanamshikilia na uongozi wahospitali kwa uchunguzi zaidi
0 comments:
Post a Comment