MTU MMOJA ANAYEDAIWA KUWA NI KIBAKA AMEUAWA KWA KUPINGWA NA KUNDI LA WANANCHI KWA TUHUMA ZA WIZI.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI“PRESS RELEASE” TAREHE 01.12.2014.
MTU MMOJA ANAYEDAIWA KUWA NI KIBAKA AMEUAWA KWA KUPINGWA NA KUNDI LA WANANCHI KWA TUHUMA ZA WIZI.
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LAEMANUEL EDWARD (29) MKAZI WA ILOMBA ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA RUFAA MBEYA BAADA YA KUSHAMBULIWA KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI FIMBO, RUNGU NA MAWE KUTOKANA NA TUHUMA ZA WIZI.
INADAIWA KUWA AWALI MNAMOTAREHE 30.11.2014MAJIRA YAALFAJIRIHUKO ENEO LA BLOCK – T, KATA YA IYELA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA MAREHEMU ALIKUTWA AKIWA KATIKA HARAKATI ZA KUIBA NYUMBANI KWAERICK ANYASWILE(53) MFANYABIASHARA, MKAZI WA BLOCK –T AMBAYE ALIPIGA KELELE ZA KUOMBA MSAADA NA WANANCHI HAO KUJITOKEZA NA KISHA KUMSHAMBULIA MAREHEMU.
INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIVIZIA WAKATI GETI LA NYUMBA HIYO LIMEFUNGULIWA NA KUINGIA NDANI KWA NIA YA KUFANYA UHALIFU HUO NA NDIPO MMILIKI WA NYUMBA HIYO ALIMUONA NA KISHA KUOMBA MSAADA. AIDHA INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKUWA NI MWIZI [KIBAKA] MZOEFU ALIYESHIRIKI MATUKIO MENGI YA KIHALIFU.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISIAHMED Z. MSANGIANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAJENGE TABIA YA KUWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUTAFUTA KIPATO CHA NJIA ZILIZO HALALI ILI KUEPUKA MATATIZO YANAYOWEZA KUJITOKEZA.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment