MCHUNGAJI : ‘ WAZAZI CHANZO MMOMONYOKO WA MAADILI KATIKA JAMII ’
Mchungaji Charles Pawa wa kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani Jimbo la Kaskazini usharika wa Kawe jijini Dares salaam amekemea tabia ya wazazi kutotilia mkazo suala la maadili kwa watoto hivyo kupelekea watoto kutokuwa na maadili yanayofaa katika jamii nchinini Tanzania.
Aidha, mchungaji huyo amesema hayo leo wakati wa akitoa sakramenti ya Kipaimara kwa watoto takribani 40 katika usharika wa Kawe jijini Dares salaam. Akitoa neno la Mungu wakati wa maadhimisho ya misa hiyo amesema hivi sasa wazazi wametupia kisogo kuwafundisha watoto kuwa maadili ya yanayofaa suala linapelekea watoto kuwa na maadili mabaya na yasiyo faa katika jamii.
Akitolea mfano, amesema aliwahi kuwepo mtoto wa kike aliyefika kanisani akiwa amevaa nusu ‘uchi’. Mchungaji alimrudisha akabadilishe nguo, alipofika tena alikuwa amevaa bora ya ile aliyokuwa nao mwanzo. Mchungaji aliamua kwenda naye nyumbani kwake, kufika pale akakuta nguo aliyovaa mama yake ni afadhali ya mtoto. Hivyo inaonesha wazi mzazi ndiye aliyemfundisha mtoto kuvaa nguo ambazo hazifai mbele ya jamii ya kitanzania.
Akizungumzia suala la kuzuka makanisa amesema kwamba duniani hivi sasa kumezuka imani za ajabu zinazofundisha mafundisho ya uongo, hivyo kuwataka waumini wa kikristo kusimama imara katika imani zao.
Kwa upande mwingine mchungaji Charles amehimiza watoto waliopata sakramenti ya Kipaimara kuhakikisha kwamba wanatenda matendo mema yatayowafanya wasiwe mbali na uso wa Mungu ikiwemo kushika amri za mungu pamoja na kufanya ibada katika maisha yao yote.
0 comments:
Post a Comment