MAMA LULU AANGUKIA KWA MZEE WA UPAKO
Mama wa staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila ameangukia katika Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo-Kibangu jijini Dar, linaloongozwa na Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako.’
Chanzo kinasema kuwa mama huyo ameamua kujikita katika maombezi na kwamba hufika kanisani hapo kila siku ya Alhamisi kwa maombezi na siku ya Jumapili kwa ajili ya ibada.
“Ni kweli kila Alhamisi mama yake Lulu huonekana hapa kanisani ambapo hupatiwa huduma ya maombezi kutoka kwa Mzee wa Upako,” kilisema chanzo.Amani lilifanikiwa kumpata mama Lulu na kumuuliza kama kweli anaabudu katika kanisa hilo ambapo alifunguka;
“Ndiyo nimeamua kumrudia Mungu baada ya kuona watu wanaendelea kutenda dhambi kila siku bila kujali kama mwisho wa dunia upo. Natumia muda mwingi katika kanisa hilo kwa maombezi.”
0 comments:
Post a Comment