MAAJABU YA SIKU ZA SIKUKUU CHRISTMAS NA MWAKA MPYA

i wish u happy chrismass and ney year


Vazi maalumu la siku ya msimu wa Christmas.
Vazi maalumu la siku ya msimu wa Christmas.
Siku za sikukuu za Christmas na Mwaka mpya ni siku ambazo watu mbalimbali ulimwenguni kote hujumuika kwa pamoja kwa  ajili ya  kusherekea kuzaliwa kwa Yesu kristo na mwaka mpya  kwa ajili ya  kumaliza mwaka na  kuukaribisha mwaka mpya.

Viongozi  wa dini husisitiza wakristo wote duniani kuungana kwa pamoja kumwabudu mwenyezi Mungu kwa kutenda matendo yanayo mpendeza mwenyezi mungu ikiwemo kusaidia wasio jiweza kutenda matendo mema.
Aidha, kinachoshangazwa katika  sikukuu hizi waumini wa kikristo pamoja na madhehebu mengine badala ya kumwabudu Mwenyezi Mungu wa mbinguni siku hizi zimekuwa zikitumika kuongeza maambukizi ya  magonjwa ya  zinaa ukiwemo ugonjwa wa UKIMWI.
Watu wengi siku hizi muhimu   huzini  pasipo kumuogopa mwenyezi Mungu. Ndoa  nyingi huingia  katika  migogoro na kupelekea nyingine hata kuvunjika. Hata  nyumba za kulala wageni (guest house ) hujaa sana watu suala linalothibisha kwamba asilimia kubwa ya watu hutumia siku hizo kuzini.
Watu wengine  hunywa pombe kupita kiasi  na kutoa lugha za matusi, Kuendesha magari  wakiwa wamelewa suala linalopelekea ajali na pengine ajali hizo kusababisha vifo. Uhalifu nao unaongezeka katika siku hizi muhimu.
Biblia inasemaje  kuhusu siku za sikukuu ?
Vitabu vya Mungu vinasisitiza watu kusherehekea sikukuu za Kristmasi na mwaka mpya kwa  amani na kwa kutenda matendo mema yanayo mpendeza mwenyezi mungu.
…………………… Kheri ya Christmas na Mwaka Mpya…………………
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: