Kocha Phiri: Simba sasa ni mabao tu

KOCHA wa Simba, Patrick Phiri amekiri kwamba straika Mliberia wa Yanga, Kpah Sherman ni bonge la mchezaji lakini akawaambia mashabiki wa Msimbazi kwamba dili zote zimetiki na safari hii wana bonge la timu ambalo halitaki suluhu ni magoli tu. Kwa kujiamini Phiri alitamka maneno haya; “Hatuna sababu ya kupata sare ama kupoteza mechi tena, tuna kikosi kizuri sasa tofauti na kile cha mwanzo.” Alisema ameamua kumsajili kiungo mshambuliaji Simon Sserunkuma kutokana na uwezo wake wa kumiliki mpira na kupiga chenga ambapo awali mshambuliaji Emmanuel Okwi pekee ndiye alikuwa akicheza soka la aina hiyo kwenye kikosi chake. “Naangalia pia uwezekano wa kuwaunganisha Okwi na Danny (Sserunkuma) kwani ni mfungaji mzuri, anafahamu goli lilipo, atatupatia matokeo pia katika mechi zetu, nafikiri kikosi changu kimekamilika.” Phiri aliongeza kuwa kutokana na aina ya uchezaji ya wawili hao kufanana itakuwa ni kazi ngumu kwa mabeki wa timu pinzani kuizuia safu yake ya ushambuliaji isifunge mabao kwani wakimkaba Okwi basi Sserunkuma atafanikisha kikosi chake kupata matokeo. Simba tayari imewasainisha Srerunkuma na beki Juku Musheed na kuwaondoa kwenye kikosi chake Warundi Amissi Tambwe na Pierre Kwizera ikiwa ni jitihada ya kuimarisha kikosi hicho kilichokumbwa na sare mfululizo msimu huu. “Nilikuwa na Okwi pekee kama mshambuliaji msumbufu, aliweza kupiga chenga na kumiliki mpira kwa muda mrefu, Simon (Sserunkuma) ni mchezaji wa aina hiyo, anajua kupiga chenga na kumiliki mpira pia. “Kwa sasa ninajiamini kwani akikabwa Okwi bado nitabakiwa na mtu wa kuweza kuleta usumbufu na kutengeneza nafasi za kufunga, ni aina ya washambuliaji niliokuwa nawahitaji kwenye kikosi changu,” alisema Phiri.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: