Jivunie kuwa mwana ludewa
Katibu Mkuu wa Bakwata Mkoa wa Mbeya, Juma Killa (wa pili kushoto) wakati wa uhai wake.
MAJANGA! Siku chache baada ya aliyekuwa Shehe Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Abubakar Mketo kufariki dunia akiwa kaburini akizika, kiongozi mwingine wa Kiislam, Katibu Mkuu wa Bakwata Mkoa wa Mbeya, Juma Killa naye amefariki dunia baada ya kuanguka chooni.
MAJANGA! Siku chache baada ya aliyekuwa Shehe Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Abubakar Mketo kufariki dunia akiwa kaburini akizika, kiongozi mwingine wa Kiislam, Katibu Mkuu wa Bakwata Mkoa wa Mbeya, Juma Killa naye amefariki dunia baada ya kuanguka chooni.
Marehemu Killa alianguka chooni nyumbani
kwake, Mtaa wa Majengo jijini hapa Desemba 7, mwaka huu na kukimbizwa
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya kwa matibabu.
Kwa mujibu wa habari za kifamilia,
marehemu alifariki dunia asubuhi ya Desemba 8, mwaka huu hospitalini
hapo baada ya hali yake kuwa mbaya tangu alipoanguka chooni siku moja
nyuma. “Baada ya kufikishwa hospitalini hali yake ilizidi kuwa mbaya.
Ilipofika asubuhi ya Desemba 8, mwaka huu alifariki dunia. Jamani, watu
wengi wanaoanguka chooni hupoteza maisha, sijui kwa nini?” alihoji
mwanafamilia mmoja huku akiomba jina lake lisiandikwe gazetini.
Ndugu huyo alisema mwili wa marehemu
ulitarajiwa kusafirishwa jana kwenda, Songwe, Chunya mkoani hapa kwa
mazishi. Mbali na kuwa katibu, marehemu pia alikuwa Mjumbe wa Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya.
Kwa upande wa Shehe Mketo yeye alifariki
dunia kwenye Makaburi ya Nonde jijini hapa alipokuwa akitoa mawaidha
katika swala ya mazishi ya mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la
Mayasa Salmini au Bibi Majuto.
Kifo cha shehe huyo kiligubikwa na
maswali mengi kwani mauti yalimkuta wakati akiwaambia waombolezaji
kuishi kwa kumwomba Mungu kwa vile mauti humkuta binadamu wakati wowote,
hata yeye anaweza kufa baada ya kumaliza mawaidha yake ambapo ghafla
alianguka kweli na kufa!
0 comments:
Post a Comment