GARI LA ASKARI LAUA MTEMBEA KWA MIGUU

MTU mmoja amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa vibaya baada ya gari kuacha njia na kuwagonga. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Isunto Mantage, alisema jana kuwa ajali hiyo ilitokea juzi, saa 2.30 usiku katika Kitongoji cha Kakunku, kilichopo Kata ya Utende, wilayani Mpanda. Alisema gari aina ya Toyota Mark II namba T 748 AAF, mali ya askari wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Mpanda, lililokuwa likiendeshwa na askari E 8834 Ephraim, liliwagonga watembea kwa miguu hao na kusababisha kifo cha mmoja wao. Alimtaja aliyegongwa na kufariki dunia kuwa ni Lumondya Mwandu (50), mkazi wa Tarafa ya Karema, aliyekuwa amekwenda katika kijiji hicho kuhudhuria mazishi ya ndugu yake. Aliyejeruhiwa katika ajali hiyo ni Jilala Lufunga (32), mkazi wa Kijiji cha Mgombe. Amevunjika mguu wake wa kulia na amelazwa katika Kituo cha Afya cha Ingongwa. Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana. Polisi bado wanaendelea na uchunguzi. Chanzo;Tanzania Daima
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: