CHADEMA YATISHIA KUIFIKISHA MAHAKAMANI TAMISEMI

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimeifikisha mahakamani Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI kufuatia malalamiko ya wagombea wa uchaguzi wa serikali za mitaa wa Chama hicho kuondolewa kwa tuhuma za kutumia mihuri ya jina la chama hicho kwa ufupi pasipo na ufafanuzi. Hayo yamezungumzwa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa kitengo cha habari wa chama hicho Tumani Makene nakusema kuwa maamuzi ya kuifikisha TAMISEMI Mahakamani yameafikiwa kufuatia Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda kuwakilisha muongozo wa uchaguzi wa serikali za mitaa bila kufanya marekebisho hali inayopelekea kuonekana kupuuzwa kwa uchaguzi huo. Ameongeza kuwa Wakati wanasheria na viongozi wa CHADEMA kutoka maeneo mbalimbali Nchini wakiendelea na taratibu za kisheria mahakamani ili kuhakikisaha haki inatendeka katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaendeshwa kidemokrasia ni vyema ofisi ya TAMISEMI ikajipanga kurekebisha utaratibu wa muongozo wa uchaguzi huo. Katika hatua nyingine Makene ameeleza kuwa endapo uchaguzi wa serikali za mitaa utavunjika kwa kukosa haki za kidemokrasia na kusababisha damu ya mtanzania ikamwagika ni wazi Mheshimiwa Pinda na Ofisi yake itahusishwa.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: