BUNGE LA VIJANA LAANZA VIKAO VYAKE KATIKA UKUMBI WA MSEKWA BUNGENI DODOMA

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeandaa Bunge la Vijana linalofanyika Mjini Dodoma kwa siku tatu, ikiwa ni jitihada la kuwajengea uwezo vijana wa vyuo vikuu nchini. Bunge hilo liloanza vikao vyake juzi linalojumuisha Vijana kutoka Vyuo Vikuu 15 vya hapa Nchini vinavyozunguka mkoa wa Dodoma. Bunge hilo linalotarajiwa kumalizika tarehe 3 Desemba, 2014, ni sehemu ya Mpango wa Elimu kwa Umma ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo kupitia mradi wake wa kuwezesha uwezo wa wabunge na watumishi unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), umelenga kuwajenga vijana kushiriki masuala ya kibunge kwa vitendo. Jumla wa wanafunzi 120 kutoka vyuo vya UDOM CBE, MIPANGO, TIA, MZUMBE St. John, VETA, Theophili kisanji - Mbeya, MKAWA, RUAHA, chuo cha kiislam Morogoro, Tumaini, na Chuo cha Sayansi Mbeya wamechaguliwa kuwa wabunge wa Bunge hilo.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: