BREEAKING NEWS>>> NDEGE YENYE WATU 162 YA AIR ASIA QZ8501 YAPOTEA

NDEGE ya AirAsia, QZ8501 iliyokuwa na watu 162 ikitokea Indonesia kwenda Singapore imepoteza mawasiliano leo asubuhi. Kati ya watu hao 162, abiria walikuwa 155, marubani 2 na wafanyakazi wa ndege hiyo 5. Watu 157 ni raia wa Indonesia, 3 raia wa Korea Kusini, 1 kutoka Malaysia na 1 raia wa Singapore. Imeelezwa kuwa kabla ya ndege hiyo kupoteza mawasiliano, rubani aliomba kubadili uelekeo wa kawaida kutokana na hali mbaya ya hewa. Ndege hiyo ilifanyiwa matengenezo kwa mara ya mwisho Novemba 16, 2014 kama ilivyokuwa imepangwa. Rubani wa ndege hiyo ana uzoefu wa saa 6,100 angani huku msaidizi wake akiwa na uzoefu wa saa 2,275. Miongoni mwa abiria 155 waliokuwa kwenye ndege hiyo, 138 ni watu wazima, 16 watoto na 1 mama mjamzito. QZ8501 imetoka Indonesia saa 11: 27 alfajiri na ilitarajiwa kuwasili Singapore saa 2:37 asubuhi.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: