BASI LAPATA AJALI MLIMA KITONGA, NI BAADA YA KUANZA KURUDI KINYUMENYUME LENYEWE

Basi la abirialenye namba za usajili T 298 BLZlikiwa linatolewa katika mtaro wa Mlima Kitonga baada ya kutumbukia. Hali hii imesababisha foleni kubwa kwa magari huku mengine yakishindwa kuendelea na safari zake. Kwa mujibu wa mashuhuda, chanzo cha gari hilo kutumbukia mtaroni ni kufuatia kupata hitilafu na hatimaye uamuzi wa kuliegesha kando ukafanyika kisha abiria wote wakashuka ili kusubiri marekebisho hayo. Haikupita muda mrefu baada ya abiria kushuka gari lilikosa balansi, likaanza kurudi kinyumenyume na kisha kuingia mtaroni. Hakuna mtu aliyefariki dunia wala kujeruhiwa katika ajali hiyo.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: