BABU WA MIAKA 62 AMCHAPA MAKONDE KIJANA WA MIAKA 29
Ule msemo wang’ombe hazeeki mainiau ule wa kiingereza ‘Old is Gold’ naweza kusema ni kama una ukweli kwa kulirejea tukio hili ambalo ni la aina yake.
Kijana wa miaka 29, Elliot Seymour ambaye damu inachemka alijikuta katika wakati mgumu kwenye uliongo wa mchezo wa ngumi pale aliposhindwa kujitutumua mbele ya mzee, kikongwe Mickey Rourke ambaye ni bondia wa zamani na pia muigizaji wa Holywood.
Katika pambano hilo ambalo lilifanyika siku ya ijumaa Marekani, kwanza lilikuwa na kiingilio kikubwa, pili lilikuwa na mvuto wa aina yake ambapo watu walihitaji kupata jibu kati ya babu wa miaka 62 na jamaa wa miaka 29 nani atamshinda mwenzake.
0 comments:
Post a Comment