ABDULHALIM HUMUD ASAINI MWAKA MMOJA COASTAL UNION
ALIYEKUWA kiungo wa Sofapaka ya Kenya, Abdulhalim Humud ‘Gaucho’ amesaini Mkataba wa miaka miwili kuichezea Coastal Union ya Tanga yenye maskani yake barabara 11 mjini hapa.
Humud ambaye aliwahi kuzichezea klabu mbalimbali hapa nchini ikiwemo
Simba amehaidi kufanya makubwa kwenye kikosi cha wagosi wa kaya ambacho kinajiwinda na michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara.
Beki huyo machachari ambaye aliondoka Simba baada ya kufungwa na anga kutokana na kutokea migogoro akaamua kwenye kujiunga na Sofapaka ya nchini Kenya.
Abdulhalim Humud 'Gaucho' kulia amesaini Coastal Union
Akizungumza na waandishi wa Habari jana,Ofisa Habari wa Coastal Union, Oscar Assenga amesema kuwa wana matumaini makubwa na mchezaji huyo ambaye alikuwa tishio kwenye vilabu mbalimbali hapa nchini alivyowahi kuvichezea.
“Sasa tumeanza kufanya mabadiliko bado mambo yatakapo kuwa mazuri zaidi tutawajulisha nini tumekifanya tena kwenye kikosi chetu “Amesema Assenga.
Hudumu tayari alishatua jijini Tanga na ameungana na wachezaji wenzake kwenye mazoezi yanayoendelea kwenye viwanja wa Disuza jijini Tanga chini ya Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi la Coastal Union Mohamed Kampira.
Wachezaji wengine waliosajiliwa kwenye kipindi cha dirisha dogo na Coastal Union ni wachezaji wa kati ambao ni Bakari Sadiq aliyekuwa nchini Denmark na sasa alikuwa akiichezea klabu ya Friends Rangers ya Dar es Salaam.
Hata kadhalika na Godfrey Wambura ambaye alikuwa ni mchezaji wa Kagera Sugar aliyekataa kwenda Simba msimu huu ikashindikana sasa ametua Coastal Union.
Kwa upande wake,Humud amesema amejisikia faraja kubwa sana kusajiliwa na Coastal Union na kuhaidi kushirikiana na wachezaji wengine ili kuweza kuipa mafanikio timu hiyo.
0 comments:
Post a Comment