WANAWAKE WATAKIWA KUHIMIZA WAUME ZAO WAFANYIWE TOHARA KUJIKINGA NA UKIMWI

Wanawake wametajwa kuwa na nafasi kubwa ya kuwashauri pamoja na kuwahimiza waume zao na watoto wa kiume kufanyiwa tohara ikiwa ni njia moja wapo ya njia ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Ukimwi. Akizungumza jana katika Kijiji cha Mwendakulima wakati wa tamasha la kutafuta kikundi bora kitakachohamasisha siku ya Ukimwi duniani Mratibu wa Ukimwi wa halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga Elibariki Minja aliwataka wanawake kutowaonea aibu waume zao badala yake wawaeleze. Alisema kama wanawake watakuwa mstari wa mbele kuwashauri wanaume ambao hawajafanyiwa tohara itasaidia sana kupunguza maambukizi ya Ukimwi pamoja na kuifanya jamii kuelimika kanda ya ziwa hususani Mkoa wa Shinyanga ambapo wanaume bado hawajawa na elimu ya kutosha kufanyiwa tohara. “Ndugu zangu wanawake naomba muwasihi na kuwahimiza waume zenu ambao bado hawajapata tohara wapatiwe ili kujikinga na Ukimwi, pamoja na kuwapeleka watoto wa kiume kufanyiwa tohara”,aliongeza Minja. Alisema kama wanaume watafanyiwa tohara itasaidia kuwapunguzia maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa asilimia 60 hivyo wanapaswa kuwahamasisha wananume ambao bado wanaona aibu ya kufanyiwa tohara. Alisema hospitali ya wilaya ya Kahama imetenga kitengo cha kufanyia tohara kila siku hivyo ni nafasi ya kila mwanamume ambaye bado hajafanyiwa kwenda kufanyiwa zoezi hilo
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: