moja ya matanuru ya tofari ambazo zimefyatuliwa na wanafunzi pamoja na walimu zikiwa zimeshachomwa tayari kwa kuanza ujenzi
madarasa ambayo yameshakarabatiwa
madarasa yasiyo karabatiwa
Mwalimu mkuu wa shule ya sekodari ya makonde Oraphy Mwinuka akitoa ufafanuzi juu ya mgomo wa wananchi
Katibu wa Mbunge Filikunjombe Bw.Stanley Gowele akiongea na wananchi wa kijiji cha Makonde
Nyumba ya Mwalimu ambayo imekarabatiwa na wanafunzi kwa kushirikiana na walimu
Madarasa yasiyokarabatiwa
kikao na mkuu wa shule kikiendelea
source habari ludewa blog
madarasa ambayo yameshakarabatiwa
Mwalimu mkuu wa shule ya sekodari ya makonde Oraphy Mwinuka akitoa ufafanuzi juu ya mgomo wa wananchi
Katibu wa Mbunge Filikunjombe Bw.Stanley Gowele akiongea na wananchi wa kijiji cha Makonde
Nyumba ya Mwalimu ambayo imekarabatiwa na wanafunzi kwa kushirikiana na walimu
Madarasa yasiyokarabatiwa
kikao na mkuu wa shule kikiendelea
Walimu na
wanafunzi wa shule ya Sekondari Makonde wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe
wameanza ufyatuaji wa matofari ili kuweza kujenga nyumba ya mwalimu wa kike
kutokana na wananchi wa kata nne zinazomiliki shule hiyo kususia kufanya
maendeleo ya ujenzi.
Akizungumza
katika ziara ya katibu wa mbunge wa jimbo la Ludewa mkuu wa shule hiyo mwalimu
Oraphy Mwinuka alisema kutokana na uhaba wa nyumba za walimu imebidi
kuunganisha nguvu za walimu na wanafunzi kufyatua matofari yatakayoweza kufanya
ujenzi huo.
Mwalimu
Mwinuka alisema shule hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo uhaba wa
nyumba za walimu hali inayosababisha kutokuwa na mwalimu wa kike kutokana na
kukosa mahala pakuishi hivyo hakuna namna ni lazima nyumba moja ijengwe ili
apatikane mwalimu wa kike.
Alisema
shule ya sekondari Makonde ni shule ya kata
ambayo iko kata ya Makonde mwambao mwa ziwa Nyasa lakini wenye dhamana
ya kuijenga shule hiyo ni kata nne ambazo ni kata ya Makonde,Lifuma,Kilondo na
kata ya Lumbila lakini mpaka sasa kata hizo hazijihusishi na ujenzi wa shule
hiyo licha ya kuwa ni ukombozi mkubwa wa kielimu kwa kata za mwambao.
“tumeshafyatua
tofari elfu kumi na tayari tumezichoma,pia tunamalizia ukarabati wa nyumba moja
ili walimu waanze kuhamia hata kama ni nyumba moja ninaimani watakaa walimu
vijana watano hatuna namna kutokana na wananchi wa maeneo haya kuwa wakaidi
upande wa elimu licha ya kuwa tumepeleka malalamiko ngazi zote lakini hakuna
majibu”,alisema mwalimu Mwinuka.
Kuhusu
wanafunzi wakike kugoma kuishi hostel mwalimu Mwinuka alisema kumekumwa na
uvumi unaotolewa na vijana wa kiume ambao si wanafunzi kutokana na tama zao za
kimwili kuwa shule hiyo inahitaji wanafunzi wawili wa kuzindikia hivyo kama
watathubutu kuishi katika hostel ni lazima wanafunzi wawili watapoteza maisha.
Alisema
mpaka sasa ni idadi ya wanafunzi wachache ndio wanaoishi hostel na hakuna
kilichotokea mpaka sasa hivyo uvumi huo wa baadhi ya vijana ni uongo hivyo
wazazi wanatakiwa kuwalazimisha watoto wao kuishi hostel ili kupunguza
uwezekano wa upatikanaji wa ujauzito kwa wanafunzi wa kike.
Ofisa
mtendaji kata wa kata ya Makonde Bw.Augan Mhagama alikiri kuwepo kwa matatizo
katika shule hiyo hasa wananchi wa kata yake na kata jirani ya Lifuma kususia
kufanya maendeleo ya ujenzi wa nyumba za walimu kutokana na kata za Kilondo na
Lumbila kutoshiriki ujenzi wa shule hiyo licha ya kuwa wanafunzi kutoka kata
hizo wanasoma shuleni hapo.
Bw.Mhagama
alisema chanzo cha migogoro ya ujenzi wa shule hiyo ni viongozi wa kata hizo
kutokuwa na ushirikiano licha ya kuwa mara kwa mara wamekuwa wakindikiwa barua
na mkuu wa shule katika mikutano ya pamoja ili kuhakikisha maendeleo
yanapatikana lakini wamekuwa wakikaidi wito huo.
Aidha katibu
wa mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe Bw.Stanley Gowele alimuagiza
katibu tarafa wa tarafa ya mwambao kuwaita watendaji wa kata zote nne pamoja na
madiwani wa kata hizo kukaa pamoja na kuona namna ya kufanya ili kuinusuru
shule hiyo.
Bw.Gowele
alisema hakuna haja ya kulumbana na viongozi wa kata hizo bali ni kukaa pamoja
na kuona namna ya kufanya kwani elimu ni ukombozi mkubwa kwa vijana hivyo
anayebisha kufanya maendeleo kwaajili ya shule hivyo achukuliwe hatua za kisheria.
Mwisho.
source habari ludewa blog
Jivunie kuwa mwana ludewa
Blogger Comment
Facebook Comment