SUALA LA KUHUSISHA TOHARA YA WANAUME NA IMANI ZA DINI LAKEMEWA VIKALI MKOANI NJOMBE

Wananchi mkoani Njombe wameaswa kutoliingiza suala la tohara ya wanaume na imani za dini kwa kuwa suala hilo ni kwa ajili ya kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI na manufaa mengine ya kiafya na si vinginevyo Hayo yamebainika wakati wa uchangiaji mada iliyowasilishwa katika kikao cha wadau wa mapambano dhidi ya vvu kilichoandaliwa na tume ya taifa ya kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) ambapo imeonekana miongoni mwa changamoto ambayo shirika la JHPIEGO lilikutana nayo wakati wa utekelezaji wa huduma ya tohara ya wanaume ni imani ya dini Mmoja wa wachangiaji hao askofu mstaafu Dkt Peter Lukumbusho Mwamasika ameeleza kuwa wapo baadhi ya watu wanadai wanaume wakifanyiwa tohara wanakuwa wamehamishwa katika imani yao ya kikristo na kupelekwa katika imani ya kiislamu jambo ambalo limepingwa vikali kuwa halina ukweli wowote Askofu huyo amesema katika kipindi hiki ambacho kila mmoja anapambana na maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi, tohara imegundulika kuwa ni moja ya njia inayopunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa waliofanyiwa tohara hivyo mwanaume aliyefanyiwa tohara imani yake ya dini inabakia pale pale Kwa upande wake mbunge wa viti maalum mkoa waIringa ambayeni mwenyekiti wa kamati ya Bunge inayoshughulikia UkimwiMh. Lediana Mng'ong'o amewatakaviongozi wa siasa kushirikishwa katikajitihada za kupambana namaambukizi ya VVU "Humu ndani siwaonimadiwani, siwaoni wenyeviti wa halmashauri, angalau nawaona wakuu wa wilaya, wenyeviti wa halmashauri ndio wasimamizi wa sheria ndogondogo ninaomba tuwashirikishe sana maana wanaushawishi mkubwa katika hili" amesema Mng'ong'o Amesema kwanafasi hii wakishirikishwa viongozi wa siasa watakuwawanapeleka taarifa hizo kwa wapigakurawao suala hilo litasaidia kuwa na mabadiliko makubwa katika jamii
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: