SPIKA MAKINDA AGEUKA MBOGO BUNGENI, NI BAADA YA RUNDO LA WABUNGE KUOMBA MUONGOZO WA SAKATA LA ESCROW
Vipaza sauti vya ndani ya Jengo la Bunge Dodoma Novemba 24 vilipaza sauti za Wabunge ambao walikuwa wakitaka Spika wa BungeAnne Makindaaruhusu kuanza kwa mjadala kuhusu tukio la mtu mmoja ambaye anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kukutwa akisambaza Ripoti ya CAG inayohusu sakata la Escrow.
MbungeJames Mbatiaalikuwa wa kwanza kuruhusiwa kuomba mwongozo huo; “… Wizi huu na usambazaji wa taarifa ya ukaguzi maalum kabla haijawasilishwa Bungeni ni vitendo vinavyotakiwa kukemewa na kutolewa tamko kali na Bunge, hivyo basi kwa kutumia kanuni ya 51 ya kanuni za Bunge toleo la mwaka 2013, naomba kutoa hoja Mheshimiwa Spika kwamba Bunge lako lisitishe shughuli zake zilizopangwa kuendelea sasa, ili Wabunge wapate fursa ya kujadili suala hili kwa kina na kutoa maagizo yanayostahili kwa Serikali …”
SpikaAnne Makindaakajibu; “… Huyo aliyehusika ameshikwa na yuko mikononi mwa Polisi sasa hivi, ofisi yangu ya Bunge imeshirikiana na Polisi kutomtoa yule mtu paka aseme hivyo vitu alivyokuwa anavisambaza vimetoka wapi, ndio kazi inayoendelea sasa hivi… hatuendeshi Bunge kwa kupiga kelele tuelewane, mtu yuko ndani sasa hivi tunavyoongea tukipata taarifa ya Polisi ndio tutajadili tunajadili nini”
Baadhi ya Wabunge hawakuridhishwa na majibu hayo ikiwemo MbungeTundu Lissu; “… Mheshimiwa Spika umeridhika kuwa hili jambo linahusu haki za Bunge ndio maana umempa Mheshimiwa Mbatia ruhusa ya kutoa hoja yake hatua inayofuata… kwa mujibu wa hiki kifungu ni kuweka kipaumbele katika shughuli nyingine zote za Bunge ili tujadili hili suala, sasa Mheshimiwa Spika hili jambo hatujadili taarifa ya kamati tunajadili haya yanayotokea ni vizuri Mheshimiwa Spika hili jambo lizungumzwe ili hii hewa chafu inayoanza kujitokeza iwe clear…”
SpikaMakindaakajibu; “… Hili suala lingekuwa limetoka tuu mtaani na kuja humu ndani tungefanya mnavyosema kwa sababu wote hatungekuwa informed, nyinyi hao na wenzenu wengine ndio mliosaidia kumshika mtu aliyekuwa anasambaza, sasa Polisi wanaendelea nasema wakishakamilisha hiyo Spika atapanga lakini bila hivyo sasa tutafanya nini Polisi wanatafuta na sisi tunazungumza humu ndani…”
Spika wa Bunge akampa nafasi MbungeOle Sendeka; “… Kwa kuwa sii busara mimi kuendelea kulumbana na kiti chako kwa uamuzi huo japo msimamo wangu ulikuwa ni ule, kwa mujibu wa maelezo uliyotoa kama unavyojua jambo hili linahitaji kutendewa haki ni jambo linalohusu uhalifu dhidi ya rasilimali za Nchi, hofu yangu Mheshimiwa Spika ni kwamba siku hiyo wakati kamati itakapowasilisha ripoti hapa na ndio siku ambayo Wabunge hao watapata nafasi ya kuiona ripoti ya CAG na ripoti pia ya kamati ya PAC…“
Sasa mashaka niliyonayo Mheshimiwa Spika ni muda gani Bunge lako litapata nafasi ya kusoma kamati ya CAG kama vyote vitawasilishwa siku hiyo na siku hiyo hiyo vikataliwa kujadiliwa wakati ambapo Wabunge hawajapata uelewa mpana juu ya ripoti yenyewe, ni kwa nini sasa usielekeze katibu wako wa Bunge ahakikishe kwamba ripoti hiyo inapatikana kwa Wabunge mapema rasmi leo badala ya kupatikana huko mitaani, ili Wabunge waweze kuisoma ripoti hii na vielelezo vyake ili waweze kuitendea haki ripoti yenyewe, vinginevyo Mheshimiwa Spika utalazimika siku hiyo ripoti itakapowasilishwa utupe siku nzima tena kwenda kujisomea na kupitia vielelezo ili tuweze kuitendea haki ripoti yenyewe…”–Ole Sendeka.
Baada ya hoja ya Mbunge huyo,Anne Makinda akajibu; “…Hili tunafanya utaratibu kusudi mpate documenti mapema ili muweze kujadili hilo ndiyo tunakubali…”
0 comments:
Post a Comment