RAIS WA UFARANSA AWAONYA MARAIS VING’ANGA’NIZI AFRIKA

Rais wa Ufaransa Francois Hollande amewapa onyo viongozi wa bara la Afrika, kwamba wanapaswa kujifunza kwa yale yaliyotokea nchini Burkinafaso na sio kung’ang’ania madarakani. Kauli ya rais Hollande imetoka katika mkutano wa nchi zinazozungumza kifaransa ,unaofanyika nchini Senegal,na kutolea mfano kwa kile kilichomkuta na kumuondoa madarakani Blaise Compaore na kutilia mkazo suala la katiba kuheshimiwa. Kufuatia kitendo hicho, raisi Hollande amesema kwamba muda wa Ufaransa kuingialia migogoro ya nchi zilizokuwa makoloni yake umekwisha kilichosalia ni kuona wale wote wanaozungumza kifaransa nchi zao zinafuata utawala wa kidemkrasia. Raisi Hollande amesisitiza kuwa nchi yake iliepusha umwagikaji wa damu na kumsaidia Compaore kuokoa jahazi lililokuwa likielekea kuzama
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: