MTOTO AZALIWA AKIWA NA MIGUU NA MIKONO MINNE HUKO INDIA

HUKO nchini India mama mmoja kajifungua mtoto mwenye miguu minne na mikono minne huku akipokelewa na wenyeji kwa furaha kubwa na kuitwa ‘Mungu Mvulana’ Mtoto huyo amepewa jina la ‘Mungu Mvulana‘ kwa kuwa kuzaliwa na viungo kama hivyo si jambo la kawaida na huchukuliwa kama mfano wa Mungu kwa jamii za kihindu. Watu walisafiri kutoka kona mbalimbali za nchi hiyo kwenda kumshuhudia mtoto huyo wa maajabu, katika mji wa Kaskazini mwa nchi hiyo walijazana nje ya eneo la Hospitali hiyo wakiwa na hamu yakutaka kumwona mtoto ambaye ana maana kubwa kwa jamii za nchini humo na wenyeji wa huko wana amini ataleta baraka katika jamii zao. Mamia ya watu walikua wamejaza nje ya Hospitali hiyo wakiimba na kusali lakini hawakuweza kufanikiwa kumwona kutokana na wingi wao huku Polisi wakitumia nguvu ya ziada kuwazuia
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: