MHESHIMIWA PROF. ANNA TIBAIJUKA BORA UJIUZULU KULINDA HESHIMA YAKO NA CHAMA

Mheshimiwa Bi. Anna Tibaijuka (Mb), Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ni moja wa viongozi wachache sana wenye ujasiri na kiongozi muwazi katika sakata zima la akaunti ya Tageta Escrow, kwani kiongozi huyu amekiri wazi kuwa amepokea fedha shilingi billion 1.6 kutoka kwa mmiliki wa kampuni ya VIP Engineering Bw. James Rugimalira. Si jambo jema kumhukumu Mheshimiwa Anna Tibaijuka, lakini siyo vibaya kumshauri kwa kuwa amekuwa muwazi katika sakata hili, basi lingekuwa jambo la maana sana kama angejiuzulu madaraka aliyonayo katika serikali ili kulinda heshima yake na ya chama tawala. Msomi yoyote yule anapofikia kuitwa Profesa na tena Waziri mwenye kushika dhamana ya nchi na wananchi yaani, Ardhi na Makazi, halafu akakubali kupokea fedha ya kiasi kikubwa hivyo bila ya kutia shaka yoyote kama ananuliwa kwa namna moja au nyingine kutokana na dhamana ya cheo chake, litakuwa ni jambo jema kwake kujiuzulu ili aonyeshe mfano bora kuwa yeye ni kiongozi mkweli na viongozi wengine wafuate nyao. Msomi aliyefikia daraja la juu kabisa tunamwona kama kiongozi anayejua wazi kuwa yeye ni mojawapo wa Mawaziri wachache ambao Wizara zao zina dhamana kubwa ya nchi, leo hii akikubali kununuliwa kiurahisi au kufanya biashara akiwa katika madaraka mazito, tuna mashaka naye ikiwa atandelea kututumikia wananchi katika Wizara ambayo pia inahusika na mipaka ya ardhi ya nchi. Watanzania tunajiuliza, hivi Mhe. Anna Tibaijuka yupo katika utumishi wa umma tena na huku akiwa Mkurugenzi wa Mashirika au Shule na miradi binafsi, ndiyo kusema cheo chake cha utumishi wa umma ndio dhamana ya biashara zake? Hivi kuna hosptali ngapi hapa nchini hazina dawa? Je wakina mama wangapi wajawazito wanafariki wakati wa kujifungua kwa ukosefu wa vifaa vya mahosptalini? Shule ngapi za serikali hazina madawati? Leo Mheshimiwa mabilioni ya fedha na kusema kuwa hakujua kama ni fedha chafu. Kwa vipi Watanzania tusiwe na mashaka naye? Professor Anna Tibaijuka anafahamu wazi kuwa amevunja sheria ya maadili ya viongozi wa umma "(Sheria namba 13 ya mwaka 1995) ambayo inawataka viongozi watoe taarifa ya zawadi wanazopokea au malipo wanayolipwa." Hivyo, sisi wananchi wenye kuiamini serikali hii hautuwezi kabisa kukubali au kuona kiongozi tena msomi anavunja dhamana ya wananchi na kumvunjia heshima mkuu wa nchi ambaye ndiye alimteua. Litakuwa jambo la busara sana Mhe. Anna Tibaijuka ujiuzulu ili kulinda heshima yako kama msomi Professor, pia kulinda heshima serikali na Chama tawala. Huwezi kutumikia ofisi mbili, yaani utumishi wa umma na biashara. Wanachi tunasikitika sana kuona katika sakata la fedha za umma mpaka baadhi watumishi wa Mungu ambao ni viongozi wa Kanisa nao wanahusika na bila ya woga. Wanapokea fedha bila ya hofu ya kujenga udini. Mungu ibariki Tanzania. MDAU
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: