ludewa yangu
MAKALA.
LUDEWA ,MANDA YANGU UMEKUMBWA NA NINI?
LUDEWA
MWANDISHI..BARNABAS NJENJEMA
Manda ni jina la kata ya Wilaya ya Ludewa katika Mkoa wa Njombe, Tanzania.kata hii ina wakazi wapatao 59,084 waishio humo. Zamani za Afrika ya Mashariki ya Kijerumani ilijulikana kwa jina la Wiedhafen ikawa kitovu cha Nyassa ya Kijerumani kabla ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Wajerumani walichagua mahali pa Wiedhafen-Manda kwa sababu ilikuwa mwisho wa njia ya misafara kati ya Kilwa na Ziwa Nyassa na kuwa na bandari asilia.
Manda iko kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa karibu na mdomo wa mto Ruhuhu, ina vivutio vingi ikiwemo ufukwe maridhawa wa ziwa Nyasa. pia kuna Kanisa la Mt Thomaso na pia bandari ya kale ya Manda-Wiedhafen.
Wenyeji wa kata ya Manda ni wamanda na lugha yao ya asili ni kimanda. Vyakula vya asili vya wakazi wa Manda ni Ugali wa muhogo na samaki. Ngoma za asili za wakazi wa Manda ni Mganda, Kihoda na ligambusi,,
mbali na historia hiyo ya kuvutia Kata ya Manda ni moja kati ya sehem iliyotoa wasomi wengi na waliokuwa na juhudi za kuleta mabadiliko ndani ya nchi na wilaya kiujumla.
0 comments:
Post a Comment