HOTUBA YA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA WAKATI WA KUHITIMISHA SHUGHULI ZA MKUTANO WA 16 NA 17 WA BUNGE
I: UTANGULIZI
a)Masuala ya jumla
Mheshimiwa Spika,
1. Leo tunahitimisha shughuli za Mkutano wa Kumi na Sita na Kumi na Saba wa Bunge lako Tukufu. Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa Rehema kwa kutufikisha salama siku ya leo.
Mheshimiwa Spika,
2. Mkutano huu ulijumuisha kujadili kazi kubwa zifuatazo:
Kwanza:Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2015/2016;
Pili:Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi wa Mwaka 2014 [The Tax Administration Bill, 2014];
Tatu:Muswada wa Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani wa Mwaka 2014 [The Value Added Tax Bill, 2014];
Nne:Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Mwaka 2014 [The Public Private Partnership (Amendment) Bill, 2014]; na
Tano:Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali wa Mwaka 2014, [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2014].
Aidha, ni hivi mapema leo Miswada11ya Sheria ya Serikali kuhusu mambo mbalimbali ilisomwa kwa mara ya kwanza.
Mheshimiwa Spika,
3. Nitumie nafasi hii kuwapongeza Waheshimiwa Wabunge wote kwa kushiriki katika Kamati ya Mipango hapa Bungeni kwa kujadili kwa kina mapendekezo yaliyowasilishwa na Serikali kuhusuMpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2015/2016.Maoni na Ushauri tuliopokea kutoka kwa Waheshimiwa Wabunge tutauzingatia wakati wa maandalizi ya Bajeti ya mwaka 2015/2016. Vilevile, niwashukuru kwa kujadili na kupitisha Miswada ya Sheria niliyoitaja hivi punde.
b)Maswali
Mheshimiwa Spika,
4. Katika Mkutano huu, Waheshimiwa Wabunge wamepata fursa ya kuuliza maswali ya kawaida na yale ya Papo Papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu. Jumla ya maswali241ya msingi na662ya nyongeza yameulizwa na Waheshimiwa Wabunge na kujibiwa na Serikali. Aidha, Maswali18ya msingi na13ya nyongeza yaliulizwa na kujibiwa kwa utaratibu wa Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu.
c)Kauli za Mawaziri
Mheshimiwa Spika,
5. Waheshimiwa Wabunge watakumbuka kuwa tarehe 17 Novemba, 2014 nilipata fursa ya kutoa Kauli ya Serikali kuhusu Mgogoro kati ya Wakulima na Wafugaji Wilayani Kiteto. Aidha, baadhi ya Waheshimiwa Mawaziri walipata nafasi ya kutoa Kauli mbalimbali za Serikali kama ifuatavyo:
i) Kauli ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuhusu taarifa zilizotolewa na Vyombo vya Habari za shutuma dhidi ya Serikali za China na Tanzania kujihusisha na Biashara Haramu ya Pembe za Ndovu na ile inayohusu Kuridhia Mkataba wa Umoja wa Afrika kuhusu Demokrasia, Uchaguzi na Utawala wa Mwaka 2007;
ii) Kauli ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii kuhusu Hali ya Dawa Nchini na Matibabu ya Saratani Nchini; na
iii) Kauli ya Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika kuhusu Mwenendo wa Soko la Nafaka na Mpango wa Ruzuku ya Pembejeo za Kilimo.
Maazimio
Mheshimiwa Spika,
6. Tarehe 7 Novemba, 2014 Waheshimiwa Wabunge walipata fursa ya kujadili na kupitisha Azimio la Bunge la Kumpongeza Mheshimiwa Anne Semamba Makinda (Mb.), Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-PF). Aidha, katika Mkutano huu Waheshimiwa Wabunge walipata pia fursa ya kujadili na kuridhia Maazimio
0 comments:
Post a Comment