DEREVA TOYO sehemu ya 8

Ilipoishia Jana "bwana wewe jemsi mbona hutulii?" Heee nilijua nitafokewa kwa kumshika kiuno bila ridhaa yake... kumbe ndio nazidi kulembesha mzigo...Afu mtoto alivaa suruali nyepesiiiiiiii mpaka raha yani.... Sasa mtoto wa kiume si nikanogewa kushika kiuno..... kumbe alikua analoku milango ya gari kisha akanigeukia na kusema "nilikua nakutega tu uingie kwenye himaya yetu.... sasa hapa hutoki na utulie hivyo hivyo nipige simu kwa mkuuu" "haaaa kwani nimefanyaje jamani?" "utajulia mbele ya safari" Aliwasha gari na kulitoa mbiooooo ENDELEAAA Nilianza kukuteyemeka huku nikijiuliza mara mbili mbili kua Iweje huyu mtoto mzuri hivi awe jangili namna hii? Maana kwa mara ya kwanza nilipomuona kiukweli huezi kutegemea kama anafanyaga kazi kama hizi.... "we judith kwani mi nina kosa gani?" "nakwambia utajulia mbele ya safari" Mungu wangu Sasa mtoto wa kiume kinyesi kinagonga boxer huku jasho chapa chapa bila hata ya kaxi ngumu "jamani judi pliz naomba unisamee... au kama ni ile pesa yako nikurudishie mamaa" "nimekwambia staki kelele" Daahh mtoto wa kiume nilikosa nguvu Maana nilitamani kuruka ila mlango umebanwa kabisaaa...... Na nadhani unamkumbuka huyu judith.... huyu ndio yule aliinilipa pesa ya upigaji picha badala ya mama yake.. na nilikua nawadai elfu 20 tu... lakini alinipa elfu 50 na kusema kua amenipa kwa kazi njema nilioifanya... nami sikua na hiana ya kupokea pongezi zangu... Sasa sijui ndio hio inanitokea puani sijui... Lakini gari ilipokua inaelekea naona kama kwenye kumbi za starehe... Na ni kweli gari iliingia hadi hotelini moja kubwa na yenye kiwango kikubwa.... Ambapo bila kuletwa na judith hapa basi nisingeweza kuingia mpaka nife... japokua kosa niliokuja nalo hapa silijui... Aliingiza gari ndani ya hotel hio kisha iitwayo MOUNT MERU HOTEL AU ( NOVO HOTEL ) Aliingiza gari kisha akalipaki maeneo ya ndani ndani sana Huku akiwa ana hasira kuliko.... Kisha akatoka na mimi pia nikatoka ila nilishindwa kukimbia kwasababu hotel yote imezungukwa na maaskari kibao..... hivyo nikikimbia naweza zua kesi mpyaa "ongoza mwenyewe kwenye ule mlango pale" Aliniambia judi kisha nikauangalia huo mlango wenyewe. ulikua ndio mlango wa kuingilia watu wa kawaida tu... "kwani nimefanyaje judi?" "hutaki kuingia au?" Nikaona kama anajisachi maeneo za kiuno nikajua Eeehh hio itakua ni bastola hivyo niliongoza mwenyewe kwenye ule mlango huku nikiangalia huku na kule kama nitaona msaada.... maana wapo watu wanatuona ila hawavuti hisia kama nimetekwa, Kwani sikua nimefungwa pingu wala nini, yani nilikua huru kabisaa Niliingia kwenye ule mlango kisha na yeye akafuata nyuma na kuchagua sehemu flani ya kukaa... alichagua sehemu ya pembezoni mwa ukuta kabisa.... "tutakaa hapa tukipata chakula huku tukimsubiri mkuu sawa?" Nikaitikia kiunyonge unyonge "saawaa" Alimuita muudumu kisha akaagiza chakula moja matata sana yaani imewekwa mixer ya kila aina. Basi mtoto wa kiume nikaanza kula lakini chakula kilikua hakishuki kooni... maana hata sijui kosa lililonileta hapa hotelini... "judi niambie basi nina kosa gani?" "nimesema kula kwanza na sitaki watu wajue kua kuna shida baina yangu na wewe" "mmhh sawa ila chakula hakishuki" "utajua mwenyewe na hiko kitakua ni chakula chako cha mwisho kwani unahitajika ufe" "what??" Niliruka na kutupa tupa vijiko huku moyo ukinienda mbio.. Mpaka nikadondoka chini na kukosa nguvu kabisa. mpaka macho yalifunga kabisa Na sikujua kilichoendelea pale BAADA YA MASAA KADHAA KUPITA na sasa nipo hospitalini sijui hili wala lile.. nilipofungua macho nilikutana na sura nzuri kidogo Sasa nilipoangalia kwa makini Kumbe alikua ni nesi wa kike NESI NI CHEO TU HAIJALISHI NI WAKIUME AU WA KIKE.... MAANA WENGI WAKIAMBIWA NENO NESI BASI WANAJUA TU NI LAZIMA AWE WAKIKE...ILA HAPANA NESI LINAKUSANYA JINSIA ZOTE.... ILA NESI NI MTU MWENYE CHEO KIDOGO HOSPITALINI....AU NI MUUGUZI WA HOSPITALI TOFAUTI NA MUUGUZI WA KAWAIDA TUNAELEWESHANA TUUUU Sasa nilimuona nesi wa kike ni mzuri kiasi... ila makalio ndio balaa "unajiskiaje jimi?" "we umejuaje jina langu?" "niliambiwa na yule dada ili tukuandikie faili" "oooohhh sasa huyo dada yuko wapi?....Alafu? pumbavu zenu yaani mumenivua nguo zangu kwanini bwana" "tafadhali kijana usirudie tena kutukana sawa? tulizivua kwa usalama wako kwani kulikua na joto sana" "huyo dada kaniona mlipokua mkinivua?" "hata kuingia humu ndani hatujamruhusu" "safi sana... na sasa hivi yupo wapi?" "yupo hapo nje tena ana hamu ya kukuona" "ooooo usimruhusu kabisa.... kwanza nipe nguo zangu Nishaapona mimi" "zile pale juu" "yaani nyie manesi ni wabaya nyie yaani mumenibakiza na boxer tu?.... hebu angalia pembeni basi mbona unanitolea macho hivyo?" "afu mtoto mdogo nanii kubwa hadi raha" "nini?" "una mchumba?" "sio mchumba tu hadi mke ninae" "mmhh muongo wewe na udogo huo?" Sasa nikawa nachungulia mlangoni ili nimuangalie huyo judi kakaa upande gani... maana sitaki nionane nae tena.... "we nesi mimi si nisharuhusiwa?" "ndio..ila mimi je?" "wewe nini sasa?
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: